Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 28.01.2020: Aubameyang, Fernandes, Cavani, Piatek, Mari, Bergwijn, Eriksen
Manchester United inafikiria kumuongezea dau kiungo wa Ureno Bruno Fernandes, 25, kabla ya Ijumaa ambayo ndiyo siku ya mwisho ya dirisha la usajili. (Guardian)
Ingawa Fernandes amejumuishwa katika kikosi cha Sporting kitakachominyana na Maritimo Jumanne jioni, hali inayoonesha kuwa uhamisho huo unaweza kuwa mgumu kukamilika. (Express)
United imeamua kumpa nafasi nyingine Alexis Sanchez mwenye umri wa miaka 31, kuonyesha uwezo wake na itamrejesha kutoka Inter Milan mwezi Juni. (Star)
Mashetani wekundu United hata hivyo wanaonyesha dalili ya kutotaka kufanya usajili katika dirisha hili la Januari hasa baada ya kupata mikingamo kwenye kuwanasa Fernandes na Edson Cavani wa PSG ambaye anaripotiwa kwenda klabu nyengine. (Independent)
Klabu ya Arsenal inatarajiwa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa Barcelona Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa miaka 30. (Telegraph)
Arsenal imebadili vigezo walivyoweka katika mkataba wa Pablo Mari, 26 baada ya ripoti ya uchunguzi wa afya yake, na kuweka wingu jeusi juu ya uhamisho huo. (Mail)
Usajili wa Mari umeshindikana na beki huyo yupo njini kurudi Brazil. (ESPN)
Atletico Madrid inakaribia kufikia makubaliano na Cavani. (ESPN)
Chelsea inamfuatilia mshambuliaji wa AC Milan Krzysztof Piatek mwenye umri wa miaka 24, ambaye anawaniwa na Tottenham wakati wakijipanga kupata mbadala wa Cavani. (Telegraph)
Raia wa Uholanzi Steven Bergwijn, 22 amekanusha kukataa kucheza katika timu ya PSV Eindhoven siku ya Jumapili na kuwa yupo kwenye mazungumzo na Tottenham. (Sky Sports)
Ingawa Bergwin aliitaka PSV kumruhusu ajiunge Spurs kabla ya dirisha la usajili halijafungwa. (90min)
Kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27, anatarajiwa kuthibitishwa kuwa mchezaji wa Inter Milan siku ya Jumanne baada ya kupita vipimo vya afya usiku wa Jumatatu. (Mail)
Manchester United, Arsenal na Tottenham wanavutiwa kumsajili mchezaji wa Ujerumani Emre Can mwenye umri wa miaka 26 akitokea Juventus.(Metro)
Borussia Dortmund wanawania pia kumsainisha Can ambaye ni kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool. (Bild - in German)
Mchezaji wa Tottenham Danny Rose, 29 na Kyle Walker-Peters mwennye umri wa miaka 22 wanatarajia kuondoka Spurs kwa mkopo kabla ya siku ya mwisho ya usajili. (Standard)
Saints wamejipanga kumsajili Walker-Peters kwa mkopo, huku wakiendelea na majadiliano kuhusu mkataba wake kama utajumuisha malipo ya paundi milioni 12 kuwa sehemu ya mkataba wake . (Mail)
Aston Villa imewasilisha dau la usajili la pauni milioni 4.2 kwa mchezaji wa zamani wa Chelsea na Liverpool, Daniel Sturridge, 30 kutoka klabu ya Uturuki ya Trabzonspor. (Talksport)
West Ham wanajipanga kumsajili mchezaji wa Tottenham na Argentina Juan Foyth, 22.
Klabu hiyo pia iko kwenye mazungumzo na Slavia Prague juu ya kiungo wa kiungo Tomas Soucek, 24. (Guardian)