Siku ya Ukimwi Duniani: Jamii inayoogopa kuonekana waasherati kwa kupima Ukimwi

Ni takribani miongo sita sasa tangu virusi vya ukimwi vilipothibitishwa kuepo. Mamilioni ya watu wamekufa kutokana na ugonjwa huo na wengine wakiwa wanaishi na virusi vya Ukimwi.

Kadri muda unavyoenda wanasayansi wakiwa wanapambana kupata tiba au hata chanjo ya virusi hivyo, watu wamejifunza jinsi ya kuishi na virusi hivyo.

Lakini unyanyapaa bado ni changamoto.

Katika jimbo la Wajir kaskazini mwa Kenya ni eneo ambalo utamaduni na dini zimechukua nafasi kubwa na kufanya jamii kuwanyanyapaa zaidi waathirika wa virusi vya Ukimwi.

Adhana husikika mara tano kwa siku kuwakumbusha watu kwenda msikitini kwa sala katika mji mzima. Eneo hili ambalo lina wakazi wengi waislamu.

Wajir iko karibu na mpaka wa Somalia, wenyeji wa eneo hilo ni wasomali ambao wana ongea lugha moja na wana tamaduni moja.

Lakini kuna mengi zaidi ambayo hayafahamiki kuhusu eneo hilo au watu hawayazungumzii.

Imesikika kuwa watu wanahangaika sana kimyakimya , kwa sababu ya kuwa na virusi vya ukimwi.

BBC imeweza kuzuru katika mji huo na kukutana na baadhi ya watu ambao wameathirika na VVU

Saadiya ni miongozi mwao ambaye anaishi katika eneo hili akiwa na watoto watatu. Mtoto wake wa kwanza ambaye anasoma ana umri wa miaka 11.

Saadiya hawezi kusimama mwenyewe. Yeye ni muhathirika wa virusi vya ukimwi. Amekuwa akipambana na umaskini peke yake kuwalea watoto.

Sijamuona au sijasikia kutoka kwa mume wangu tangu mwaka 2013. Hicho ndicho kipindi ilinibidi nimpeleke mwanangu hospitalini pia.

Madaktari walivyompima walimkuta ameathirika pia na virusi vya ukimwi. Walinipima mimi pia na kunikuta nimeathirika.

Saadiya anasema kuwa alishtuka sana kusikia hiyo taarifa. Lakini hakuwa amejiandaa kuwa angekutana na changamoto hiyo.

Mara tu tatizo hilo linapogunduika kwa umma, anatengwa. Nililazimika kuhama kutoka eneo ambalo nililokuwa ninaishi mpaka kuja kuishi hapa.

Majirani zangu walikuwa wanawatukana watoto wangu . Nilikuwa nashindwa kuazima kitu chochote kutoka kwa majirani zangu; hakuna mtu ambaye alikuwa anajali kuwa ninaweza kuishi au kufa.

Walikuwa hawawezi kuchangia maji na mimi katika kisima. Hata sasa hapa sio nyumbani kwangu. Wananiongelea sana na walikuwa wanawapiga watoto wangu wakiwaona.

Huwa anatumia muda mwingi kukaa peke yake na mara nyingi na huwa anapokea wageni mara chache.

Lakini Saadiya anasema alikuwa anakubali kila kitu ambacho kilikuwa kinamkuta. Ni watoto wangu ndio nilikuwa nawahofia.

Watoto wangu wanasoma katika shule ya msingi ya umma; mtoto mdogo yuko shule ya awali.

Lakini walifukuzwa kuhudhuria masomo ya dini na wanakijiji.

Hata watoto wa jirani yangu walikuwa wananitukana sana kila siku kutokana na kile ambacho huwa wanasikia kutoka kwa wazazi na jamii inayonizunguka.

Lakini nashukuru kwamba bado wanaruhusiwa kwenda shule.

Jamal pia ana virusi vya ukimwi. Yeye anaishi mjini Wajir na yeye alikuwa anakumbana na ubaguzi kutokana na hali yake.

Sehemu ya kwanza niliyoishi wakati nilipooa, nilifukuzwa. Walinifukuza hata nyumba niliyoamia baada ya ile .

Baada ya miezi miwili au mitatu baada ya kuhamia nyumba mpya, habari kuhusu mimi zilisambaa kutoka kwa watu ambao walikuwa wananijua kabla kuhusu hali yangu. Taarifa zikamfikia mwenye nyumba na kunifukuza. Nilifukuzwa kwa sababu ya hali yangu ya afya.

Siwezi kumuomba mtu kitu chochote, si chakula wala malazi yani si kwa chochote.

Yani hawataki kusikia hilo neno ukimwi, ninalipa kodi lakini walikuwa hawataki hata pesa yangu.

Jamal alilazimishwa kukonda. Alipoteza marafiki zake na familia yake mara tu walipogundua kuwa ana virusi vya ukimwi.

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa idadi ya watu ambao wana virusi vya ukimwi nchini Kenya , kuna maambukizi mapya takribani 52 000 kwa watu rika zote.

Hii ikijumuisha maambukizi mapya yapatayo 44000 ya vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 49 .

Maambukizi ya watoto wadogo chini ya miaka 14 yalikuwa chini ya 8000 mwaka jana.

Licha ya kuwa Wajir kuwa eneo lenye watu wengi nchini humo, bado rekodi zinaonyesha kuwa kiwango cha maambukizi iko chini kwa 0.2 % .

Ingawa kuna hofu kuwa inawezekana kuna watu wameathirika lakini wanshindwa kujitokeza kwa kuogopa unyanyapaa ambao umetawala katika eneo hilo.

Mawasiliano yameongezeka na maambukizi ya virusi vya ukimwi yameongezekan.

Kuna watu wengi ambao hawajapima na tumewaona, kwa mfano mwezi huu tu tuna rekodi ya maambukizi mapya ya watu nane. Hivyo ukimwi upo katika jamii hii lakini unyanyapa unawafanya watu wasiende kujua hali zao.

Uzinzi umekatazwa katika kitabu kitakatifu cha Quran.

Katika jumuiya ya kiislamu , waislamu wanahofia kuwa kama wakienda kupima virusi vya uimwina ndugu zao wakawaona, watahusisha kuwa wamefanya uzinzi na unyanyapaa utakuja na jamii kuwatenga.

Watu wachache ambao wameweza kuzungumza mbele za watu kuhusu hali zao na kuchukua jitihada za kuelimisha watu kuhusu virusi vya ukimi.

Inabidi tujaliane, huwa tunaandika miradi ya kuomba ufadhili ili tuendelee kusaidia wengine.

Tunawaeleza kuwa wote sisi ni familia moja. Na katika dunia hii tuna uwezo wa kuishi miaka mingi tukiwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Kuna wengi ambao wamenyanyapaliwa lakini bado wapo hai. Hivyo inatupasa kunywa dawa kama tulivyoshauriwa na madaktari.

Lakini inaonekana ni rahisi kusema kuliko kutenda. Haswa pale waathirika wengi wanaposhindwa kumudu kununua chakula cha siku.

Katika jamii ya wasomali, watu kujitokeza kwa umma kusema hali zao ni jambo la nadra sana.

Wafanyakazi wa afya wana kazi ya ziada ili kuwashawishi watu kusema hali yao katika jamii kwa sababu wanakuwa wakali sana.

Kila siku kuna simulizi za kutisha kuhusu unyanyapaa wa wagonjwa wa ukimwi katika jamii ya wasomali.

Wengine huwa wanatafuta msaada bila mafanikio.

Kuna hatua kadhaa zimechukuliwa ilikupunguza ubaguzi dhidi ya watu walioambukizwa virusi vya ukimwi lakini naona hatua hizo zinaenda polepole na safari kuwa ya maumivu makali.

Mpaka kila mtu akiwa anauelewa kuhusu virusi vya ukimwi basi wale wenye virusi vya ukimwi inabidi wajitegemee wenyewe.

Hii ikimaanisha ishi mwenyewe na upweke.