Matokeo ya sensa Kenya yazua mjadala

Chanzo cha picha, Reuters
Takwimu za sensa za idadi ya watu nchini Kenya zimetolewa na kusababisha kutoelewana kwa baadhi ya makundi ya watu kuhisi kuwa hayakuwa sahihi.
Sensa hiyo iliyofanyika hivi karibuni ilipata idadi ya watu nchini humo kuwa milioni 47.6 , idadi ambayo ni kubwa kwa milioni tisa tofauti na mwaka 2009.
Lakini baadhi ya miji kukiwa na upungufu wa idadi ya watu.
Matokeo hayo yanaweza kuleta ubishani mkubwa kwa sababu kuna umuhimu wa kiwango cha wakazi kujulikana kwa ajili ya serikali kuweza kutumia vizuri fedha inazozipata.
Kwa nini ni muhimu kujua idadi ya watu?
Idadi ya watu nchini Kenya imeweza kuleta tofauti nyingi katika makundi ya watu kwa kuangalia tamaduni zinazoshabihiana , wanavyohusiana na vyama vya kisiasa .
Serikali imetoa takwimu zote kwa kuangalia na utamaduni wa watu katika taifa hilo , lakini kila mabadiliko ya idadi ya watu katika baadhi ya maeneo tayari yamezua mjadala.
Matokeo ya utafiti yanaweza kuathiriwa au kudhoofishwa na malalamiko yaliyotolewa na makundi ya kisiasa au uwasilishi wa rasilimali.
Katika eneo moja kaskazini mashariki ya mpaka wa Ethiopia na Somalia, sensa imebainisha kuwa idadi ya watu imepungua na hivyo kuwafanya viongozi wa kisiasa wa maeneo hayo kubisha ili kuendelea kutafuta namna ya kubaki na ufadhili waliokuwa wanapata zamani kutokana na idadi yao kuwa kubwa, na jambo hilo ndio linawafanya kuhoji uhalali wa utafiti uliofanyika.

Chanzo cha picha, Getty Images
Eneo ambako idadi yawakazi wake wana asili ya Somalia.
Tahwimu pia zilibaini kuwa kuna utofauti mubwa wa kijinsia katika eneo hilo, kuna wanaume wengi zaidi ya wanawake, hii ikiwa inakadiriwa kuwepo kwa matukio mengi ya vifo wanawake au wanaume wasiooa kuhamia maeneo hayo kwa ajili ya ajira.
"Takwimu hii ilitolewa wiki iliyopita sio ya kweli na haiwezi kukidhi malengo," alisema Aden Duale, Kiongozi wa wangeni katika bunge na mwanasiasa ambaye anawakilisha jumuiya ya wasomali nchini Kenya.
Alidai kuwa kwa kawaida wanaume Wasomali huwa wanaoa mke zaidi ya mmoja hivyo idadi ya watoto lazima itakuwa kubwa vilevile idadi ya wanawake lazima iwe kubwa.
Hata hivyo ofisi ya takwimu nchini Kenya imetetea uhalali wa idadi ya watu.
Sensa ni nini na inafanyaje kazi?
Sensa ni namna serikali inavyokusanya taarifa kuhusu watu wake.
Kiujumla huwa inahusisha taarifa kama takwimu za watu , makazi yao, jinsia , kabila na dini zao. Sensa kwa kawaida huwa inafanyika kila baada ya miaka 10.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni kazi kubwa ambayo inahusisha kuangalia katika ramani kila nyumba katika nchi na kuzitembelea ili kupata majibu ya maswali yao.
Baadhi ya mataifa tayari yamehamia kwenye mfumo wa kidigitali ambapo watu wanajaza mtandaoni na kuachana na kufanya utafiti wa kuandika kwa peni na karatasi,.
Nchini Kenya ,sensa huwa inafanyika kwa watumishi wa serikali kutembelea nyumba moja baada ya nyingine, kurekodi taarifa katika tablet na kutuma taarifa katika takwimu kuu ya pamoja.
Kukusanya taarifa mara nyingine kuna ugumu wake, jamii inakuwa haiiamni serikali yake na hivyo kuwa wagumu kutoa taarifa zao binafsi.
Ni namna gani serikali inatumia taarifa hizi?
Matokeo ya sensa yanaweza kuleta manufaa makubwa kwa dunia na raia wake.
Nchini Kenya , haisaidii serikali katika ugawaji wa ufadhili peke yake kwa kuhusisha kiwango cha watu lakini pia uainisha mipaka ya eneo huwa inawekwa kutokana na takwimu za sensa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nchi ambayo imegawanyika , ndio inaweza kufanya sensa kuwa jambo gumu zaidi.
Ethiopia imeahirisha kufanya sensa mara mbili tangu mwaka 2017 kwa sababu ya maandamano na vurugu za kikabila.
Kwa mfano watu wa Sidama kusini mwa Ethiopia wanafanya kampeni ya kupata jimbo lao wenyewe.
Nigeria ina historia ndefu ya kuwa na sensa ambazo zinakuwa na ubishani mkubwa, walikuwa wafanye sensa nyingine mwaka 2016, lakini haikufanyika kutokana na uhaba wa fedha na ukosefu wa vifaa ulisababisha kutonyika.
Na nchini Lebanon, haijafanya sensa tangu mwaka 1932. Hii ni kutokana na ubishani wa hata wa wawakilishi wa bunge.
Unaweza kusoma pia:












