Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 02.10.2019: Willian, Dembele, Son, Sanchez, Longstaff, Allegri, Kane, Costa

Kocha wa zamani wa Juventus Mtaliano Massimiliano Allegri, 52, anajifunza Kingereza akilenga kuhamia katika Ligi ya Primia, hususani klabu ya Manchester United. (Guardian)

Manchester United wanataka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Lyon Moussa Dembele, 23, na kiungo wa Newcastle Sean Longstaff, 21, mwezi January. (Star)

Barcelona wanajipanga kutuma tena ofa ya usajili kwa kiungo wa Chelsea na Brazil Willian, 31, ambaye bado hajasaini mkataba mpya na Chelsea, na alionao unaisha mwishoni mwa msimu. (Mundo Deportivo via Express)

Mshambuliaji wa Burnley Jay Rodriguez, 30, anahusishwa na tetesi za kushtukiza za uhamisho kuelekea klabu ya Inter Milan mwezi Januari. (Calcio Mercato via Sport Witness)

Mshambuliaji wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez, 30, amesema "ameyapata tena mapenzi yake ya kucheza mpira" baada ya kujiunga kwa mkopo na Inter Milan. (Eurosport)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp atasikitishwa sana iwapo watalazimishwa kucheza mchezo wa marudiano wa Kombe la Corabao dhidi ya MK Dons kama adhabu ya kumchezesha mchezaji asiyestahili. (Times)

Mshambuliaji wa Tottenham na Korea Kusini Son Heung-min, 27, amesema kuwa alitaka kuihama klabu hiyo mwaka 2016 lakini akashawishiwa kubaki na kocha Mauricio Pochettino. (Goal)

Kocha wa Newcastle United Steve Bruce amewauliza kwa hasira wachezaji wake iwapo wanataka kuendelea kuichezea klabu hiyo kwa moyo mmoja baada ya kupokea kichapo cha goli 5-0 dhidi ya Leicester. (Telegraph)

Mlinzi wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya England Rio Ferdinand amependekeza kuwa mshambuliaji wa klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya England Harry Kane, 26, ahame klabu yake iwapo anataka kushinda mataji makubwa. (Mail)

Beki wa England England Kieran Trippier, 29, amesema "sikujiuliza mara mbili" juu ya kuihama Tottenham yenye maskani yake Kaskazini mwa London na kujiunga na klabu ya Atletico Madrid ya Uhispania. (Football.London)

Atletico Madrid wamefanya mazungumzo na klabu ya Al Rayyan ya Qatar juu ya usajili wa mshambuliaji Diego Costa. (AS Diario via Mail)

Everton wameshindwa kumsajili mshambuliaji kinda wa Ureno Rafael Leao licha ya kutoa kitita cha euro milioni 30. Klabu ya Lille ilimuuza mshambuliaji huyo AC Milan. (Tuttosport via Liverpool Echo)

Tetesi bora za Jumanne

Beki wa Manchester United na timu ya taifa ya Ivory Coast Eric Bailly sasa kusalia nje ya uwanja mpaka mwezi Januari. Baily, 25, alipata majeraha ya goti kwenye mchezo wa kujiandaa na msimu dhidi ya Tottenham. (Sun)

Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 21, anatarajiwa kukataa ofay a kuchezea timu ya taifa ya Nigeria na badala yake kuelekeza nguvu zote kwa England iwapo ataitwa na kocha Gareth Southgate katika michezo ya kufuzu Euro 2020 dhidi ya Jamhuri ya Czech na Bulgaria. (Telegraph)

Kocha wa zamani wa Arenal, Arsenal Arsene Wenger yupo kwenye orodha ya makocha wanaowaniwa na miamba ya Italia AC Milan kurithi mikoba ya kocha Marco Giampaolo. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund amefichua kuwa hadhani kuwa nyota wao kinda Jadon Sancho, 19, akisalia klabuni hapo kwa muda mrefu. Sancho kutoka England alikuwa akihusishwa na Man United katika dirisha la usajili lililopita. (Kicker, via Mail)

Beki wa Tottenham Jan Vertonghen, 32, ambaye makataba wake unaisha mwishoni mwa msimu amesema kuwa anaweza kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (London Evening Standard)

Spurs tayari wameshafungua mazungumzo na Mbelgiji huyo Vertonghen, ili kumuongezea mkataba. (Mail)