Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Miaka milioni mbili iliyopita ilikuwa rahisi kujifungua
Kuzaliwa kwa binadamu kunapitia mchakato mrefu sana, wenye maumivu, unaohitaji msaada wa wataalamu na mpaka mtoto azaliwe, siku nzima inaweza kuisha.
Lakini ni kwa nini viumbe hai wengine kama ya sokwe huwa wanajifungua kiurahisi kwa masaa tu na bila kuhitaji msaada wowote?
Katika kufuatilia jibu la swali hili, Wanasayansi wamekuwa wakiangalia namna binadamu wanavyojifungua watoto wao.
Binadamu walioishi miaka milioni mbili iliyopita walikuwa na maisha rahisi sana, kwa mujibu wa historia za hatua za ukuaji wa binadamu.
Kwa binadamu wa kale aliyeishi miaka milioni 1.95 iliyopita huko Afrika kusini, historia inaonyesha namna uzaliwaji wake ulivyokuwa rahisi, mtafiti Dkt Natalie Laudicina anaeleza.
"Mtoto alikuwa anaweza kutoka kwa kwa nafasi kwa kichwa kuanza na mabega kufuata na hakukuwa na ugumu wowote wa mtu kujifungua," mtafiti huyo aeleza.
Siku hizi mambo yako tofauti kabisa, kichwa cha mtoto ni kikubwa na hivyo inamuwia mama vigumu kujifungua kiurahisi.
Watoto wachanga wanalazimika kupitia hatua kadhaa kabla ya kuzaliwa, badala ya kujifungua kwa kutoka tu kama ilivyokuwa awali.
Utafiti uliofanywa kwa baadhi ya wanawake unaonesha kuwa kuna mfanano wa awali -
Kuna mabadiliko ya zaidi ya awamu sita ndani ya miaka milioni tatu ya mageuzi ya binadamu- watafiti wanaweza kujua kwa nini uzazi wa kipindi cha awali una utofauti na uzazi wa sasa.
Hii sio tatizo, lakini zoezi la kujifungua linazidi kuwa gumu kadri ya miaka inavyozidi.
Mtaalamu wa binadamu wa kale kutoka chuo cha Boston anasema kuwa binadamu wa kwanza 'Lucy' alikuwa anapata wakati mgumu zaidi wakati wa kujifungua zaidi ya 'A. sediba', ugumu wakati wa kujifungua na hao wote waliishi miaka milioni iliyopita.
"Kuna tabia ya kufikiria juu ya uvumbuzi wa kuzaliwa kwa mwanadamu kama mabadiliko kutoka kwa 'rahisi', kuzaliwa kama ape kwa 'ngumu', kuzaliwa kisasa
Kwa kawaida uvumbuzi wa binadamu na mabadiliko yake tangu alipokuwa na muonekano wa sokwe na sasa kuwa na wakati mgumu wa kujifungua," anasemaDr Laudicina, aliandika katika jarida la Plos One.
Majibu ya maswali haya kwa uzazi wa sasa yanaonekana kuwa na changamoto.
Wanawake wa sasa wakitaka kujifungua lazima wapitie uchungu wa kupita kiasi kwa wa zaidi ya saa 20