Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Spurs yajikita kwenye nne bora
Klabu ya Tottenham Hottspurs imejika kwenye nafasi zuri ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi Brighton & Hove Albio, katika mchezo wa ligi kuu ya England
Spurs walilazimika kusubiri dakika za kuku kuingia bandani kupata goli pekee la ushindi lilofungwa na kiungo wake Christian Eriksen kwa shuti la mbali kwa ushindi huu Spurs wanasalika katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 70.
Na Baada ya mchezo mwalimu wa Spurs Mauricio Pochettino amesema kiungo wake Christian Eriksen atafanya mazungumzo ya kuongeza mkataba mrefu baada ya ligi kumalizika, Kumekuwa na tetesi Eriksen anatakiwa na Real Madrid.
Na Katika mchezo mwingine Wanajeshi wa Njano Watford wakiwa nyumbani Vicarage road walienda sare ya goli 1-1 na Southampton,
Goli la mshambuliaji wa Saint Shane Long, limeweka rekodi ya kuwa goli la haraka zaidi kuwahi kufungwa katika ligi ya England likifungwa katika sekunde ya 7.69
Goli hili la long linavunja rekodi iliyoweka miaka 19 iliyopita na Ledley King mlinzi wa kati aliyekuwa anaichezea Spurs amabe yeye alifunga katika sekunde 9.82.
Mshike mshike wa kuwania kuwa katika nafasi ya nne bora inaendelea tena leo Mashetani wekundi Man United watakuwa nyumbani Old traford kuwaalika the Citizens Manchester City.