Mahakama Kenya yabatilisha uamuzi unaoshurutisha shule kuruhusu Hijab

Wasichana wa shule Kenya

Chanzo cha picha, AFP

Muda wa kusoma: Dakika 2

Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya imetupulia mbali agizo la kuzitaka shule kuwaruhusu wanafunzi wa kike wa Kiislamu wavae Hijabu kama sehemu ya sare.

Hijabu ni kitambaa ambacho huvaliwa na wanawake wa kiislamu kama ishara ya kujistiri.

Lakini sasa Mahakama kuu imetoa uamuzi kuwa shule zina haki ya kuweka sharia zao.

Ni uamuzi wa daima, lakini ambao huenda ukaeneza suitafahamu baina ya sharia za shule nchini Kenya dhidi ya Imani katikadini ya kiislamu.

Wazazi wa wasichana watatu walikuwa wameishitaki mahakamani shule moja eneo la Isiolo, inayodhaminiwa na Kanisa la Kimethodisti, ambayo iliwatimua wasichana hao walipokataa kuvua hijabu kichwani kwa sababu ya muongozo wa dini ya Kiislamu.

vazi la kidini kwa wanawake waislamu

Chanzo cha picha, AFP/GETTY/REUTERS

Hata hivyo mahakama ya rufaa ikageuza maneno na kuwakubalia wanafunzi kuvaa hijabu.

Lakini kanisa kwa niaba ya shule ikakata rufaa, na sasa mahakama ya juu Zaidi imetoa uamuzi kuwa kila shule ina haki ya kuamua sharia zake, ikiwemo mavazi ya sare za shule.

Hatua hiyo imepokewaje?

Uamuzi huo wa mahakama umezua maoni tofauti katika mitandao ya kijamii huku wengine wakitaka wizara ya elimu nchini Kenya kuingilia kati suala hilo.

Kukataa kwao kulikwenda kinyume na sheria za shule, Kesi ilipofika mahakamani, mahakama kuu ilikubaliana na uamuzi wa shule.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Juma moja tu lililopita, Waziri wa Elimu Kenya aliiagiza shule nyingine jijini Nairobi, kumruhusu shuleni mwanafunzi aliyekataa kunyoa nywele zake alizozifuga Rasta, kwani katika dini yake ya Rastafari, waumini kwa kawaida hawanyoi nywele.

Mataifa mengine yaliyopiga marufuku hijab

Baadhi ya mataifa ya Afrika magharibi yamepiga marufuku hijab kwa sababu za kiusalama.

Mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo wa kundi la Boko Haram, katika eneo la kaskazini mwa Nigeria yameifanya taifa hilo kuweka marufuku ya vazi hilo la kidini.

Mataifa mengine kama vile Cameroon, Chad na Niger pia yalifuata mkondo huo wa Nigeria kwa sababu yanakabiliwa na tishio la usalama kutoka kwa wanamgambo hao.

Mwanamke akiwa amevaa Hijab
Maelezo ya picha, Mwanamke akiwa amevaa Hijab

Kaskazini mwa Afrika, Tunisia ni moja ya kati ya mataifa yaliyoweka vikwazo dhidi ya vazi la hijab.

Uturuki iliwahi kupiga marufuku wanawake kuvaa hijab katika vyuo vikuu vya umma.

Barani Ulaya, Ufaransa ni taifa la kwanza kupiga marufuku wanafunzi waislamu kuvaa hijab au mavazi mengine ya kidini katika shule za umma.