Marufuku ya matatu kuingia katikati ya jiji la Nairobi yawalazimu wakazi kutembea mwendo mrefu

Msongamano wa watu wanaotembea kuingia katikati ya mji
Maelezo ya picha, Watu walilazimika mwendo mrefu kuingia katikati ya mji
Muda wa kusoma: Dakika 3

Mamlaka za jiji la Nairobi zimeanza kutekeleza sheria inayopiga marufuku magari ya usafiri wa umma maarufu kama matatu kuingia katikati ya jiji kuanzia leo.

Hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka inalenga kupunguza msongamano wa magari.

Sheria hiyo mpya ilianza kutekelezwa mapema alfajiri ya leo ambapo maafisa wa trafiki wa kaunti ya Nairobi walikuwa wakizuia matatu kuingia sehemu ya katikati ya jiji.

Baadhi ya maafisa hao waliokuwa wamejihami kwa silaha za moto wamepelekwa katika vituo vipya vilivyowekwa nje ya jiji

Maafisa hao waliweka vizuizi vya barabarani katika eneo la Muthurwa, barabara ya Murang'a, Fig Tree A, barabra ya Desai, barabra ya Ngara, Hakati, Railways na kituo kikuu cha mabasi katikati ya jiji.

Amri yao kwa wahudumu wa matatu ilikuwa wazi: "Simama! Hakuna kuendesha gari kupita hapa."

Maafisa hao walikuwa wanayazuia matatu yanayojaribu kuingia jijini kurejea yalikotoka au kutafuta njia nyingine mbadala.

Watu watembea kuelekea kazini
Maelezo ya picha, Watu watembea kuelekea kazini

Katika mzunguko wa uwanja wa michezo wa City, polisi waliegesha gari lao katika sehemu moja ya barabara ili kuyafungia magari yote ya usafiri wa umma yanayotumia barabara ya Jogoo.

Hali ilikuwa hiyo hiyo katika barabara kuu za Thika na Limuru , ambako wasafiri wengi walilazimika kushukia stendi ya Fig Tree katika eneo la Ngara .

Katika eneo la katikati ya jiji ambako barabara nyingi hushuhudia msongamano mkubwa saa za asubuhi hali ilikuwa tofauti.

Hapakuwa na matatu katika maeneo ya Koja, Odeon, Kencom, GPO, OTC, Commercial, Ronald Ngala , Ambassadeur, barabara ya Murang'a pamoja na vituo vingine vya mabasi ya River Road.

kituo cha mabasi

Waliyo athiriwa zaidi na marufuu hiyo

  • Wahudumu wa magari ya usafiri wa umma ambao watapoteza wateja,
  • Wafanyikazi wa jijini ambao watalazimika kutembea mwendo mrefu kufika mahali pao pa kazi
  • Wafanyibiashara ambao wamekuwa wakitumia matatu kuingiza na kutoa bidhaa zao kutoka katikati ya jiji sasa watalazimika kutafuta usafiri mbadala.

Alhamisi iiyopita wahudumu wa matatu walikuwa wameapa kukaidi amri hiyo hali iliyozua hufu ya wahudumu hao kukabiliana na maafisa wa kuweka usalama

Wamilikiwa matatu wanahoji kuwa Gavana wa jimbo la Nairobi Mike Mbuvi Sonko amekimbilia kuweka sheria hii mpya bila kuwashirikisha wadao wote husika katika suala hilo.

Hatua hii imepokelewaje?

Wakenya walitumia mitandao ya kijamii kueleza ghadhabu zao.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Wengine walisema hawapingi suala la kuondoa msongamano wa magari katika eneo katikati ya jiji kwani ni kawaida katika miji mingine mikuu duniani.

Wanasema tofauti ya miji hiyo na Nairobi ni kwamba kuna mfumo imara wa kuhakikisha watu waaingia jijini bila changamoto zozote.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Kumekuwa na hofu kuhusiana na uwezo wa stendi mpya zilizotengwa kwa magari zaidi ya 20,000 ambayo yanahudumu katika jiji kuu la Nairobi.

"Wanachama wangu hawako tayari kuondoa magari yao jijini hadi pale sekali ya kaunti itakapofikia matakwa yao," mwenyekiyi wa chama cha wafanyikazi wa matatu(AMW) Clement Njuguna alisema siku ya Jumamosi.

Bwana Njuguna aliongeza kuwa "Nafasi katika stendi hizo mpya ni ndogo mno kwa magari yetu na haijafikia viwango vyetu."

Hata hivyo waziri wa uchukuzi wa kaunti ya Nairobi, Mohamed Dagane ametetea uamuzi huo akisema stendi hizo szitatumika kama sehemu ya kuchukua na kuwashukisha abiria na wala siyo sehemu ya kuegesha magari hayo.

Magari ya usafiri wa umma
Maelezo ya picha, Magari ya usafiri wa umma kutoka mikoani pia yameathiriwa na sheria hiyo mpya

Suala la usalama wa vituo hivyo limekuwa likiKwa upande wake mwakilishi wa chama cha wamiliki wa magari, Simon Kimutai amelalamikia utekelezaji wa sheria hiyo mpya.

Anasema ''Si magari ya uchukuzi wa umma yanasababisha msongamano wa magari katika sehemu ya katikati ya jiji''

Juhudi ya kupiga marufuku magari ya usafiri wa umma kuingia katikati ya jiji zilitibuka miaka iliyopita na ililazimika kusitishwa ili kutoa nafasi ya mashauriano kati ya washika dau wakuu.