Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wauguzi 16 wa ICU wapata ujauzito kwa wakati mmoja
Wauguzi 16 wana ujauzito kwa wakati mmoja katika hospitali ya Mesa,Arizona.
Asilimia 10 ya wahudumu wa chumba cha uangalizi maalum wameanza kugundua ongezeko la wingi wa wauguzi kuwa wajawazito.
Katika mkutano wa habari,wanawake walitania kuwa lazima kutakuwa na kitu kilichosababisha hali hiyo au labda walikuwa mapumziko ya sherehe za noeli pamoja(christmas)
Katika kundi hilo la wauguzi wajawazito ,wa kwanza anatarajiwa kujifungua mwezi septemba na wa mwisho mwezi januari.
Rochelle Sherman ambaye ana mwezi mmoja tu aweze kujifungua alisema kuwa hawakuwa wamegundua kuwa wako wajawazito wangapi mpaka walipoanzisha kikundi katika mtandao wa kijamii wa facebook.
"Inavyoonekana ni kama tulikuwa tumekubaliana lakini imetokea tu"
Hata hivyo wameshukuru kwa wafanyakazi wenzao kuingia kwenye idara yao na kuanza kuwasaidia kazi ambazo wanawake wajawazito hawawezi kuzifanya kama vile kumuhudumia mgonjwa mwenye ugonjwa wa kuambukiza kama kifua kikuu na kuwahudumia wagonjwa wa saratani.
Wafanyakazi hao watafanya sherehe ya pamoja ya kukaribisha watoto wao'babyshower'wiki ijayo kabla hawajaenda kwenye mapumziko ya uzazi.