Njia ya kuwaokoa vijana 12 waliokwama kwenye pango Thailand inatafutwa

Thai cave

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Timu ya uokozi

Wavulana kumi na wawili pamoja na kocha wao mmoja waliokwama katika pango moja lililojaa maji nchini Thailand wamepokea chakula cha kwanza tangu walipokwama pamoja na dawa kitakachodumu kwa siku kumi.

Wazamiaji saba, pamoja na daktari mmoja na nesi mmoja watakaokuwa wanafuatilia hali za afya zao humo pangoni , wameungana na na kikundi kilichomo pangoni upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya kugundua kuwa timu hiyo iko hai mwanzoni mwa wiki hii.

Wazamiaji kwa sasa wanabangua bongo ni kwa namna gani iliyo bora zaidi watakavyo fanikisha kulitoa kundi hilo pangoni hadi seheme ya usalama.

Mvua nyingi zinazonyesha zinaashiria kiwango cha maji kujaa na kuhatarisha maisha ya watu waliomo pangoni pamoja na mifuko ya hewa waliyonayo mahali waliko kama mateka.

Thai cave
Maelezo ya picha, Hali ilivyo pangoni Thailand

Wavulana hao waligunduliwa siku tisa baada ya kuingia pangoni humo huko katika jimbo la Chiang Rai kufuatia mafunzo ya mpira waliyokuwa wakifanya na kujikuta wakikwama pangoni kutokana na kina cha maji kuongozeka kulikosababisha na mvua nyingi zinazonyesha.

Mapema wiki hii, Maafisa wa serikali nchini Thailand waliwaambia waandishi habari kwamba wakoaji wameanza na zoezi la kuchunguza afya za kundi hilo pamoja na matibabu, na pia kuwaburudisha vijana hao na kuarifu kuwa hakuna hata mmoja mwenye afya mbaya miongoni mwa waliokwama pangoni.

Wavulana hao walipewa chakula chepesi kwa kuanzia ambacho ni rahisi kusagika tumboni, chenye kuongeza nguvu kwa haraka , chenye wingi wa vitamini na madini mwilini. Chini ya uangalizi makini wa madaktari, anaarifu Apagorn Youkonggaew ambaye ni mkuu wa vikosi maalumu vya uokozi nchini Tailand wakati wa mkutano baina yake na waandishi habari.

Thai cave

Chanzo cha picha, Fcaebook

Maelezo ya picha, Timu ya watu kumi na tau iliyokwama pangoni nchini Tailand

Kwanini hawawezi kuogelea na kutoka nje?

Inaaminika kuwa miongoni mwa vijana hao waliokwama wote hawajui kuogelea, na kusababisha ugumu wa zoezi la uokozi.

Mapema, Jeshi nchini Thailand limearifu kuwa wavulana hao kuna haja kuwa wanapaswa kujua kuogelea na kuzamia ama wasubiri hadi miezi minne hadi mafuriko hayo yapungue na hivyo kufanya zoezi hilo kuwa rahisina kutoka nje ya mapango, hii ina maana kwamba chakula kinapaswa kupelekwa mapangoni humo kwa muda wote huo.

Waziri wa mambo ya ndni nchini Thailand Anupong Paojinda alisisitizia suala la dharula la uhamishaji wavulana hao, huku akiongeza kuwa anataarifa ya mvua kuwa nyingi siku kadhaa zijazo kutokana na utabiri wa Bangkok Post.

Majaribio yanafanywa ili kupunguza hatari ya mafuriko zaidi chini ya mapango kwa kusukuma maji kutoka mfumo wa chini ya ardhi, amearifu waziri huyo.

Simu moja imeshgushwa mpaka mapangoni ili kuwawezesha wavulana hao kuzungumza na familia zao.

Naye Gavana wa Chiang Rai, Narongsak Osoththanakorn, amethibitisha kutokuwepo kwa hatari yoyote inayowakabili timu hiyo ya mpira wakati wa uokozi, na kwamba hawatafanya haraka yoyote ya kuwatoa wavulana hao bila uangalifu na kwamba kama kuna yeyeote aliye hatarini kwa namna yoyote atakuwa wa kwanza kutoka mapangoni humo.

Thai cave
Maelezo ya picha, Ramani ya kuelekea pangoni

Gavana huyo amearifu kuwa kumekuwa na wito wa kujengwa kwa miundo mbinu katika ujia unaoelekea katika eneo walilomo timu hiyo.

Mamlaka za Thailand zimetoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuwezesha harambee ya ununuzi wa vifaa vya uokozi vinavyoendana na umri wa wavulana hao ili kuepusha hatari ya mfumo wa njia ya hewa ambayo inaweza kutokea ikiwa vifaa hivyo vya kuwezesha kupumua ikiwa haviwatoshi wakati wakipita katika eneo lenye mafuriko njiani kuelekea eneo salama.

Kwenye mkanda wa video wavulana hao wanaonekana wakiwa wameketi na tochi zao mikononi eneo la juu la maji, wakijibu mwito wa wazamiaji kwamba wote wako salama na kwamba wana njaa kali.

Walifikaje eneo hilo?

wavulana hao wenye umri kati ya miaka kumi na mmoja na kumi na sita, na kocha wao mwenye umri wa miaka ishirini na tano walipotea mnamo June ishirini na tatu mwaka huu. Inaaminika kuwa waliingia pangoni wakati lilipokuwa kavu na mara ghafla mvua kubwa ilinyesha na kuziba eneo la kutokea, lakini maji machafu na matope na uchafu, yalizuia njia ya kutokea na kuongeza kiza pangoni .

Wazamiaji walilazimika kutembea katika miamba iliyochongoka,sehemu nyembamba wakati wa kiza. Walimaliza safari yao ngumu na kuifikia pwani ya Pattaya iliyofura, na kuwakuta wavulana na kocha wao karibu umbali wa mita 400.