Je huenda hilo likawa suluhu ya kupungua kiwango cha uzazi?

Akina mama wa Romania wanaweza kupata fursa ya kustaafu mapema, kama muswada uliowasilishwa bungeni utapitishwa.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la Mediafax, wabunge kutoka chama tawala cha kijamii Democratic Party, pamoja na chama cha Alliance of Liberal na Democrats wametoa ushirikiano katika kusukuma toleo la marekebisho ya sheria ya pensheni nchini humo.
Waraka huo unasema wanawake wataweza kustaafu miaka miwili mapema kwa ajili ya kila mtoto aliyezidi miaka kumi.
Mediafax inasema muswada huo uliandaliwa kwa sababu wanawake wengi wanazidi kuacha kazi au kuahirisha kuwa na watoto kwa sababu za kiuchumi.
Shirika hilo limedokeza kuwa kiwango cha uzazi cha Romania kimeshuka na kinazidi kuwa chini, huku idadi ya watoto wanaozaliwa ikiendelea kushuka hadi chini ya laki mbili kwa mwaka. Hii inamaanisha kwamba idadi ya watu inazidi kupungua kwa waromania watano kila saa.
Malezi na kazi Afrika
Changamoto za kazi na malezi zinasumbua zaidi familia hasa kina mama, kwani kuna sheria ya likizo ya uzazi ila bado wajiuliza baada ya likizo, mama anaporudi kazini hali ya malezi kwa mtoto inakuwaje?
Wazazi wengine huacha watoto na wadada wa kazi.
Lakini kutokana na matukio mbalimbali ya unyanyasaji wa watoto, watoto huanza masomo yao ya chekechea wakiwa na umri mdogo.
Nyakati nyingine wakiwa na umri wa miaka miwili tu, kwani wazazi wao kufanya kazi mbali na nyumbani.

Chanzo cha picha, TARA MOORE
Umri wa kustaafu kwa wanawake nchini Romania unategemea mwaka wao wa kuzaliwa, lakini kwa akina mama waliozaliwa baada ya mwaka wa 1955 inakadiriwa kuwa ni miaka 60.
Shirika la taifa la mfuko wa pensheni wa Umma linasema itafikia miaka 63 kwa mwaka 2030.













