Mbunge wa Tanzania Stephen Ngonyani maarufu Profesa Maji Marefu ameaga dunia

Chanzo cha picha, @Stephen Ngonyani Facebook
Mbunge wa Korogwe Vijijini kupitia CCM Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu ameaga Dunia.
Taarifa zinasema Maji marefu alikuwa amelazwa Dodoma kwa matibabu na June 20 akahamishiwa katika hospitali ya taifa ya muhimbili kabla mauti kumkuta.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na uongozi wa hospitali ya Muhimbili.
Ikumbumkwe kuwa mapema tarehe sita mwezi June mwaka huu Profesa Maji marefu alifiwa na mke wake aliyekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa Muhimbili.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Stephen Hilary Ngonyani amezaliwa mwezi mei mwaka 1956, amekuwa mbunge wa Korogwe vijijini tangu mwaka 2010.
Alizidi kupata umaarufu katika ulimwengu wa siasa.
Katika harakati zake za kutetea wananchi Bungeni, mwaka 2016 Ngonyani alitoa hoja ya kupandisha bei ya petrol na kushusha bei ya sukari ili kuwasaidia zaidi watanzania hasa wa hali ya chini.
Kabla ya hapo Ngonyani alifahamika Zaidi kama profesa Maji marefu ambapo alikuwa ni mganga na mtaalamu wa tiba za asili.
Shughuli zake za uganga zili zungumziwa katika mitandao na hata baadhi ya majarida.
Nchini Kenya Stephen Ngonyani ama profesa Maji marefu, aliwahi kuweka kituo cha kazi zake za tiba Kenya na alifanya kazi kama mganga wa kienyeji.
Alimulikwa mnamo mwaka 2010 baada ya kuhusishwa katika mgogoro wa familia ya aliyekuwa mwana siasa maarufu na tajiri.
Taarifa za mazishi yake bado hazija wekwa wazi, lakini Tayari bunge la Tanzania limetoa Taarifa kuwa wata kaa na familia ili kushiriki katika kuratibu mazishi.














