Mafuriko yasababisha maafa makubwa Ugiriki

Mafuriko hayo yanatajwa kuwa mabaya zaidi kwa kipindi cha miaka ishirini
Maelezo ya picha, Mafuriko hayo yanatajwa kuwa mabaya zaidi kwa kipindi cha miaka ishirini

Vikosi vya uokoaji nchini Ugiriki vinasema takriban watu kumi na nne wanahofiwa kufariki baada ya mafuriko makubwa kutokea karibia na mji mkuu Athens.

Wanasema wanatarajia kuopoa miili ya watu wengi zaidi.

Maji yamezingira kila kona ya mji kutokana na mvua kali.

Nyumba za makaazizile za biashara pamoja na barabara zimeharibiwa vibaya.

Meya wa mji wa Nea Peramos uliopo Magharibi mwa Athens amesema juhudi za haraka za uokoaji zinahitajika.

Mafuriko hayo yanatajwa kuwa mabaya zaidi kwa kipindi cha miaka ishirini iliyopita.