Messi afunga ndoa na mpenzi wake wa utotoni

Chanzo cha picha, Reuters
Nyota wa soka nchini Argentina Lionel Messi amemuoa mpenziwe wa utotoni nyumbani kwao katika kile kilichotajwa kuwa harusi ya karne.

Chanzo cha picha, AFP
Sherehe hiyo kati ya Messi mwenye umri wa miaka 30 na Antonela Rocuzzo mwenye umri wa miaka 29 ilifanyika katika hoteli ya kifahari katika mji wa Rosario.
Nyota wa soka na watu maarufu walikuwa miongoni mwa wageni 260 huku mamia ya maafisa wa polisi wakipelekwa kushika doria.

Chanzo cha picha, Ronald Grant
Messi na Rocuzzo walikutana wakiwa watoto wa miaka 13 kabla ya yeye kuelekea Uhispania.

Chanzo cha picha, Reuters
Miongoni mwa wageni katika harusi hiyo ya Ijumaa ni wachezaji wenza Luis Suarez, Neymar, Gerrard Pique na mkewe Nyota wa muziki Shakira.
Idadi kubwa ya wageni walisafiri kuelekea Rosario katika ndege za kibinafsi.

Chanzo cha picha, AFP
Gazeti la Argentina la Clarine limeitaja harusi hiyo kuwa harusi ya mwaka na harusi ya karne.








