Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waasi waonyesha wasiwasi kusitishwa mapigano nchini Syria
Makundi ya waasi nchini Syria yameonesha kutoridhishwa na kusitishwa kwa mapigano kunakosimamiwa na Urusi na Marekani ambapo kusitishwa huko kunatarijiwa kuanza Jumatatu jioni.
Makundi hayo yanatakiwa kusema kama watajiunga kwenye makubaliano hayo ama la.
Kuna madai kuwa moja ya kundi la waasi la Ahrar al-Sham watakataa kusitisha mapigano hayo.
Kiongozi wa kikundi kingine cha waasi mjini Alepo amesema kuwa wanakubali kuondoa uhasama na kuruhusu misaada lakini ana wasiwasi na makubaliano.
Mashambuzli ya ndege za Syria na Urusi yameendelea siku ya jumapili katika mji wa Alepo na Idlib.
Zaidi ya watu 100 wameuawa katika mashambulizi yaliotekelezwa siku ya jumamosi.