Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Biden:Ushahidi unahitajika, Fethullah Gulen kuhukumiwa
Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amesema serikali ya Uturuki inahitaji kutoa ushahidi zaidi ili kuhakikisha mhubiri wa kiislam anayeishi Nchini Marekani, anarejeshwa ili ahukumiwe Uturuki baada ya kushitumiwa kuhusika kwenye mapinduzi yaliyoshindwa mwezi uliopita.
Katika kikao chake na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kilichofanyika Ankra, Bwana Biden amesema Marekani haina nia ya kumlinda Fethullah Gulen.
Kwa upande wake bwana Erdogan amesema kuwa mhubiri huyo anapaswa kurudishwa Uturuki haraka iwezekazavyo.
Bwana Gulen amekanusha kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi.