Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Polisi watibua ndoa ya wapenzi wa jinsia moja Nigeria
Maafisa wa polisi nchini Nigeria wanawasaka watu wawili wanaotuhumiwa kwa kuandaa ndoa ya wapenzi wa jinsia moja katika mji wa kaskazini wa Nigeria wa Sokoto,msemaji wa polisi ameiambia BBC.
Mmiliki wa nyumba ambayo sherehe hiyo ilifanyika wikendi iliopita amekamatwa lakini washukiwa wakuu bado hawajapatikana.
Mapenzi ya jinsia moja nchini Nigeria ni kinyume na sheria.
''Polisi wameanzisha uchunguzi mkali kwa lengo la kuwafungulia mashtaka watu hao wawili kwa kuhusika katika tendo linalokiuka maumbile'',aliongezea.
Watu wengine waliokuwa katika sherehe hiyo walitawanyika wakati polisi walipowasili katika eneo la sherehe hiyo.