Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Liverpool 'yainyoa' Arsenal
Liverpool ilitoka nyuma na kufanikiwa kuilaza Arsenal katika mchuano mkali uliopigwa katika uwanja wa Emirates.
Theo walcot aliifungia Arsenal bao la kwanza katika dakika ya 31 mda mfupi baada ya kukosa mkwaju wa penalti.
Lakini Phillipe Coutinho alisawazisha kwa kufunga bao zuri kupitia mkwaju wa adhabu kabla ya Adam Lallana kufunga bao la pili mda mchache tu baada ya kipindi cha pili kuanza.
Coutinho alifunga bao la tatu na Sadio Mane akaongeza la nne kabla ya Alex Oxlaide Chamberlain kufunga bao zuri la pili naye Calum Chambers akafunga bao la tatu kupitia kichwa.