Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Polisi wavunja maandamano mjini Addis Ababa
Polisi nchini Ethiopia wamevunja maandamano mjini Addis Ababa na kuwakamata watu kadhaa.
Waandaanaji kadha nao walijeruhiwa.
Mwandishi wa BBC aliwaona vijana kadha wakiingizwa ndani ya malori ya polisi
Maandamano zaidi yameripotiwa kutoka sehemu zingine kutoka eneo kubwa zaidi nchini Ethiopia la Oromia ukiwemo mji wa Addis Ababa.
Wakereketwa wa jamii ya Oromo wamesema polisi wamewaua ma mia ya jamaa zao na maelfu kukamatwa tangu maandamano hayo yalipoanza mwaka jana mwezi Novemba .
Serikali imetupilia mbali idadi hiyo na kusema waandamanaji hao si halali.