Tetesi za soka Ulaya Ijumaa tarehe 19.11.2021: Ibrahimovic, De Jong, Pickford, Tolisso, Gavi, Xhaka

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City inakaribia kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 24, kwa pauni milioni 75. (El Chiringuito, via Sun)
Mshambuliaji wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic anaonekana amejipanga kuendelea kubakia katika klabu hiyo ya Serie A. Mchezaji huyo raia wa Sweden mwenye umri wa miaka 40, ambaye alijiunga na klabu hiyo Januari mwaka jana, atakuwa nje ya mkataba msimu huu lakini atasaini mkataba mpya utakaodumu hadi Juni 2023 . (Football Italia)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wako tayari tu kumtoa mshambuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette, 30, kwa mkataba mfupi tu ili kuendelea kubakia naye ndani ya klabu hiyo kwa msimu mwingine (Athletic - subscription required)
Chelsea wanajiandaa kumhamisha kiungo wa kati wa Barcelona mwenye umri wa miaka 17 Gavi. Mhispania huyo ambaye mkataba wake unaendelea hadi 2023, ameondoa kipengele cha kumuachilia cha paumi milioni 42 huku Chelsea wakiangalia jinsi ya kumhamisha. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Tottenham Antonio Conte ana nia ya kusaini mkataba na mlindalango wa Everton Muingereza Jordan Pickford, 27. Muijtalia huyyo anasemekana amepangwa kukaba nafasi ya Mfaransa Hugo Lloris mwenye umri wa miaka 35, ambaye anamalizia mwaka wa mwisho wa mkataba wake katika Spurs. (Mirror)
Spurs pia wameonyesha nia kwa kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ufaransa Corentin Tolisso lakini wanaweza kukabiliwana na ushindani kutoka kwa Internazionale ambao pia wanamvuizia mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 27. (Kicker - in German)

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati huo huo, Chelsea huenda wasimtoe kwa mkopo winga Mmorocco Hakim Ziyech, 28,mwezi Januari . (Telegraph)
Roma wanaweza kufungua tena mazungumzo ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Arsenal na Uswiss Granit Xhaka, 29. (Corriere dello Sport, via Football 365)

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakala wa mshambuliaji wa Red Bull Salzburg ya Ujerumani na Liverpool anamlenga Karim Adeyemi, 19, amekutana na Paris St-Germain. (Sport 1 via Express)
Newcastle United imepokea uungaji mkono katika nia yake ya kumsaka mlinzi wa Bayern Munich Niklas Sule. Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 26-Mjerumani anataka kuondoka upande wa Ligi ya Bundesliga side na mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu. (Bild, via Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United imekataa taarifa kwamba inamtaka meneja Mfaransa Zinedine Zidane, 49, achukue nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer katika Old Trafford. (Athletic - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi mkuu wa Ubelgiji Roberto Martinez anaamini mshambuliaji wa timu yake Eden Hazard ni mwenye "masikitiko" katika Real Madrid. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka amekuwa akihusishwa na klabu za zamani Chelsea na Newcastle. (Metro)
Meneija wa Burnley Sean Dyche anasema kiungo wa safu ya Kati -nyuma Muingereza James Tarkowski, 28, ana "mawazo ya wazi " na "malengo" licha ya kwamba klabu za Newcastle, West Ham na Tottenham zinamtaka. (Burnley Express)












