Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 20.04.2021:Vieira, Watkins, Bale, En-Nesyri, Sule, Dzeko

Mchezaji wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira ,44, yuko katika orodha ya makocha wanaosakwa na Crystal Palace ikiwa Roy Hodgson,73, ataondoka mkataba wake utakapomalizika msimu huu wa joto. Mfaransa huyo hakuwa akifanya kazi tangu alipoondoka Nice mwezi Desemba. (Athletic, subscription required)

Tottenham Hotspur wanamtaka meneja wa Red Bull Leipzig Mjerumani Julian Nagelsmann,33- kuchukua nafasi ya Jose Mourinho, ambaye alifutwa kazi Jumatatu. (Mail)

Kocha wa zamani wa Spurs Mourinho alipinga kusajiliwa tena mshambuliaji wa Wales Gareth Bale,31 kwa mkopo kutoka Real Madrid mwezi Septemba. (Telegraph, subscription required)

Crystal Palace ni klabu ya hivi punde kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na England Ainsley Maitland-Niles. Leeds United na klabu ya Monaco ya Ufaransa pia zinamfuatilia nyota huyo aliye na umri wa miaka 23, ambaye amekuwa West Bromwich Albion kwa mkopo tangu mwezi Januari. (Mirror)

Liverpool wanamtaka mshambuliaji wa Aston Villa na England Ollie Watkins, 25, ambaye alivunja rekodi ya usajili wa klabu hiyo ya Midlands miezi minane iliopita alipojiunga nayo kutoka Brentford kwa kima cha paundi milioni 28. (Football Insider)

West Ham United wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsaini Youssef En-Nesyri kutoka Sevilla, licha ya Liverpool na Manchester United kuhusishwa na mshambuliaji huyo wa Morocco alie na umri wa miaka 23. (La Razon - in Spanish)

Everton wameanza mazungumzo na mlinzi Seamus Coleman kuhusu jukumu la ukufunzi wakati atakapomaliza kucheza. Mkataba wa Colman 32, kutoka Jamhuri ya Ireland utaendelea hadi Juni mwaka 2022. (Liverpool Echo)

Chelsea imeongeza juhudi za kumsaka mlinzi wa Bayern Munich Niklas Sule, baada ya meneja Thomas Tuchel kupatia kipaumbele usajili wa Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 25, anayecheza safu ya kati na nyuma. (Athletic, subscription required)

Barcelona wako tayari kumuachilia Riqui Puig ,21, aondoke klabu hiyo msimu huu wa joto na wamepokea ofa kutoka klabu za Ligi Kuu za England, Italia, Ujerumani na Ureno zinazotaka kumunua kiungo huyo wa kati wa Uhispania aliye chini ya miaka 21. (Sport - in Spanish)

Aston Villa wanapanga kuwasiliana tena na mchezaji wa Werder Bremen Milot Rashica,24, baada ya kumkosa winga huyo wa Kosovo msimu uliopita. (Football Insider)

Bayern Munich wamejitolea kwa udi na uvumba kumsajili kiungo wa kati wa Rennes na Ufaransa wa chini ya miaka-21 Eduardo Camavinga, 18, ambaye pia ananyatiwa na Real Madrid. (France Football)

Mshambuliaji wa Roma na Bosnia Edin Dzeko,35, anasakwa na Inter Milan msimu huu wa joto baada ya klabu hiyo ya Italia kushindwa kumleta San Siro mwezi Januari. (Calcio Mercato - in Italian)