Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 07.03.2020: Zidane, De Bruyne, Sterling, Skriniar, Zidane, Cantwell, Matic

Zinedine Zidane

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mkufunzi wa Rea Madrid Zinedine Zidane

Juventus iko tayari kumpatia Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane mkataba wa £7m ili kumvuta mchezaji wake wa zamani kuchukua uongozi katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu. (Mail)

Arsenal huenda ikalazimika kumuuza nahodha wake na mshambuliaji matata Pierre-Emerick Aubameyang, 30, mwisho wa msimu huu kutokana na mahitaji ya mshahara wake. Mshambuliaji huyo wa Gabon ameanzisha mazungumzo kuhusu kandarasi mpya na anataka kulipwa mshahara wa £300,000- kwa wiki . (Mail)

Real Madrid imeanzisha tena mpango wake wa kutaka kumnunua kipa wa Man United na Uhispania David de Gea, 29. (Sun)

Kevin De Bruyne
Maelezo ya picha, Kiungo matata wa Manchester City

Manchester City iko tayari kuanzisha mazungumzo kuhusu kandarasi mpya na kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin De Bruyne, 28, na mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 25. (Mail)

Manchester City itaimarisha ombi lake la kutaka kumnunua beki wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 25, mwisho wa msimu huu baada ya kufeli walipowasilisha ofa ya 60m euros (£52m). (Calciomercato - in Italian)

Nemanja Matic

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa Man United

Tottenham itashindana na Liverpool pamoja na Manchester United ili kumsajili kiungo wa kati wa NorwichTodd Cantwell, 22. (Express)

Manchester United haijatumia kifungu cha nyongeza ya mwaka mmoja cha kandarasi ya mchezaji wa Serbia Nemanja Matic ambayo inakamilika mwisho wa msimu. (Manchester Evening News)

Chelsea ipo katika mazungumzo ya kumsaini kinda wa Ujerumani mzaliwa wa Ufaransa anayeichezea klabu ya VfL Bochum Armel Bella-Kotchap, 18. (Sun)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 32, amehusishwa na uhamisho wa Inter Milan na klabu nyengine , sasa anataka kusalia katika klabu ya Stamford Bridge na anasubiri mkataba. (Evening Standard)

Olivier Giroud

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud ameamua kusalia katika klabu hiyo

Kinda wa Chelsea na Scotland Billy Gilmour, 18, analengwa na klabu za Real Madrid na Barcelona. (Star)

Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham anatarajia kurudi uwanjani mwezi huu baada ya kuuguza jeraha na ana matumaini ya kuwa tayari kuichezea England mwezi huu katika mechi ya kirafiki dhidi ya. (Evening Standard)