Genk kukipiga na Liverpool ligi ya mabingwa Ulaya

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema mabingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya wanapaswa kujitahidi wanapocheza ugenini ili kuepuka kuondolewa mapema kwenye michuano.

Liverpool ilichapa Tottenham katika fainali msimu uliopita lakini ilipoteza michezo yote mitatu ugenini na Napoli msimu huu.

Liverpool ni ya pili kwenye kundi E na inacheza dhidi ya Genk nchini Ubelgiji siku ya Jumatano ambapo Samatta na Mo Salah watakutana uso kwa uso.

'' Mwaka jana tulikuwa na bahati kwa namna ambavyo kundi lilikuwa gumu na kushuhudia tukipoteza mara tatu ugenini na bado tukawa na nafasi ya kupita,'' alisema Klopp.

''Hilo halitatokea mwaka huu'' ni tofauti kabisa.

''Tunajua kihistoria si jambo jema kwa kile tulichofanya (katika michezo ya ugenini hatua ya makundi) katika miaka michache iliyopita, kwa ujumla ligi ya mabingwa ilikua nzuri sana.

'' Tulifanya mambo mazuri na kwa wakati sahihi lakini hatuegemei mambo haya. Tunajua tunapaswa kuweka jitihada na kujaribu tena na tena na tena mpaka tutakapofanikiwa.''

Liverpool ina alama tatu kutokana na michezo miwili baada ya kuipiga Red bull Salzburg katika uwanja wa Anfield.

Kurejea kwa Salah

Mohamed Salah amerejea kwenye kikosi cha Livepool baada ya kupona kifundo cha mguu

Mshambuliaji huyo wa Misri, 27 alipata jeraha hivyo kukosa mechi ya Liverpool na Manchester United siku ya Jumapili.

Hii ni mara ya pili kwa Genk na Liverpool kukutana .

Katika michuano iliyopita ya Ulaya Genk ilikutana na Chelsea Stamford Bridge mwaka 2011-12 katika hatua ya makundi, na kutoka sare ya 1-1 nyumbani na baadaye kupoteza bada ya kuchapwa na Chelsea mabao 5-0.