Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 23.10.2019: Sancho, Alena, Mandzukic, Ibrahimovic, Morelos, Diaz

Chanzo cha picha, EPA
Mchezaji wa zamani wa Liverpool wa safu ya kati Dietmar Hamann anasema kuwa amepata fununu kwamba Reds "wanahamu sana" ya kumsajili winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19. (Sky Germany - via Mirror)
Tottenham wanampango wa kumnunua kiungo wa kati wa Uhispania wa miaka 21 Carles Alena kutoka Barcelona mwezi Januari. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Manchester United huenda ikaongeza juhudi ya kumsajili Mario Mandzukic, 30, baada ya mshambuliaji wa Juventus na Croatia kupunguza masharti ya marupu rupu yake. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid imemwambia kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City Brahim Diaz, 20, kwamba inataka kumuuza kama sehemu ya kuondokeana nae kabisa. (Mail)
Mchezaji wa safu ya kati ya Real Isco, 27, amekubali kuwa mmoja wa wachezaji watakaoondoka klabu hiyo mwezi January mwakani. (Mail)
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Paris St-Germain na Juventus, Zlatan Ibrahimovic,38, anataka kurejea katika ligi kuu ya Italia, Serie A.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa zamani wa Uswidi katika klabu ya LA Galaxy unakamilika mwisho wa mwaka huu. (CalcioMercato)
Barcelona imepinga madai kuwa imeilipa Atletico Madrid euro milioni 15 kumaliza mzozo kati yake na klabu hiyo kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28. (Sport)
Juventus na Atletico Madrid ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia beki wa West Brom Nathan Ferguson, 19. (Sun)

Chanzo cha picha, Rex Features
Meneja wa chuo cha mafunzo ya soka ya Manchester United Nicky Butt anasema klabu hiyo inawachezaji wengi ambao wanaweza kufuata nyayo za mshambuliaji Marcus Rashford na kuleta mabadiliko katika kikosi cha kwanza. (Goal)
Crystal Palace itamenyana na Aston Villa katika juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Colombia Alfredo Morelos, 23, kutoka Rangers mwezi Januari. (Express)

Chanzo cha picha, SNS
Kocha wa zamani wa Tottenham Glenn Hoddle anadai kuna wachezaji "wanne au watano" katika kikosi cha Mauricio Pochettino ambao wanajua wataondoka katika klabu hiyo mwanzo wa msimu ujao. (Express)
Beki wa zamani wa Manchester United Jaap Stam ambaye anatarajiwa kujiunga na Feyenoord msimu huu wa joto anasema kuwa alikataa nafasi aliyopewa ya kuwa meneja wa Newcastle. (Voetbal International - in Dutch)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle imepinga madai hayo na kusisitiza kuwa haijawahi kuwa na mpango wa kumuajiri mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi. (Chronicle)
Tetesi Bora Jumanne
Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, anatakiwa na Crystal Palace na huenda akajiunga na klabu hiyo ifikapo mwezi Januari. (Daily Star)
Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino, anasema kuwa anahofia kufutwa kazi kutokana na matokeo mabaya ya klabu hiyo (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Real itaipatia Spurs kiungo wao wa kati wa Uhispania Isco, 27, na mshambuliaji wa Jamuhuri ya Dominica Mariano Diaz, 26, katika juhudi ya kupata saini ya Eriksen. (El Desmarque - in Spanish)
Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema anataka kusalia klabu hiyo maisha. (Marca)
Mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 22, anakaribia kutia saini mkataba mpya wa kusalia Stamford Bridge baada ya kufunga mabao manane katika ligi ya Premia msimu huu. (Daily Star)












