Tetesi za soka Ulaya Jumatatu tarehe 23.09.2019: Xavi, Keane, Mourinho, Balotelli, Sottil, Hysaj

Kiungo wa kati wa zamani wa Barcelona Xavi, ambaye ni meneja wa timu ya Qatari ya Al-Sadd, anasema kuwa itakuwa ni tatizo kwake kuwaongoza wachezaji wenzake wa zamani kama vile Lionel Messi, Luis Suarez na Sergio Busquets katika Nou Camp. (Ara, via Goal)

Tottenham imetuma ujumbe kumchukunguza mchezaji wa kimataifa wa timu ya vijana waliochini ya miaka 21 wa Italia winga wa Fiorentina Riccardo Sottil ambaye ni mchezaji wa kiwango cha juu huku wakionyesha nia ya kumchukua kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 . (Express)

Matumaini ya Chelsea ya kusaini mkataba na mchezaji wa Napoli Elseid Hysaj msimu ujao yanaweza kugonga mwamba huku klabu hiyo ya Italia ikiwa tayari kurefusha mkataba na kijana huyo kutoka Albania mwenye umri wa amiaka 25. (Express)

Meneja wa Everton Marco Silva ameutuma ujumbe umchunguze zaidi mshambuliaji wa timu ya RB Leipzig Yussuf Poulsen, mwenye umri wa miaka 25. (Express)

Roy Keane amesema kuwa "ameshtushwa na kusikitishwa " na namna klabu yake ya zamani Manchester United walivyoshindwa 2-0 na West Ham Jumapili. (Sky Sports, via Evening Standard)

Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 26, aliyejiunga na timu hiyo ya Italia kutoka Manchester United msimu huu, anasema kuwa kocha wa klabu hiyo Antonio Conte ni mtu ambaye ''anamsaidia kila siku na humpa motisha''. (Metro)

Meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho anasema golikipa wa Uhispania David de Gea, mwenye umrui wa miaka 28, alikuwa na "bahati kidogo'' kupata mkataba mpya mzuri na klabu hiyo . (Sky Sports, via Mail)

Mashabiki wapatao 1,000 wa timu ya Valencia waliandamana kabla ya mechi dhidi ya Leganes, kwa kutofurahishwa na namna mmiliki mwenza wa Salford City Peter Lim, na rais Anil Murthy anavyoendesha a klabu hiyo ya ligi ya La Liga . (Marca)

Mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli,ambaye anaweza kuchezea Brescia dhidi ya Juventus Jumanne , anasema amefanya ''kazi kubwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu uliopita " kuliko'' kipindi cha muongo mzima wa kazi yake'' huku kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 akilenga kupata nafasi katika kikosi cha nchi hiyo kitakachocheza kombe la Euro 2020. (Football Italia).

Tetesi za soka Jumapili

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Tottenham Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 27, na mchezaji wa kiungo cha kati Eric Dier, aliye na miaka 25, wapo juu kwenye orodha ya Manchester United ya wachezaji wanaolengwa kwa uhamisho. (Star)

Inaarifiwa Manchester United ina hamu ya kumsajili meneja wa Paris St-Germain Thomas Tuchel kama anayewezekana kuichukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer iwapo matokeo hayatoimarika (Mail)

Wakati huo huo, Manchester United ina hamu ya kujadili kuongezwa muda kwa mkataba wa mchezaji wa kiungo cha kati anayeichezea timu ya taifa ya Ufaransa pia Paul Pogba na wakala wa mchezaji huyo wa miaka 26, Mino Raiola katika wiki chache zijazo. (ESPN)

Zidane pia amedai kwamba kushindwa kwa Real Madrid kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, na mchezaji wa kiungo cha kati wa Ajax Donny van de Beek, aliye na umri wa miaka 22, msimu huu wa mjira wa joto ni uamuzi wa bodi na sio wake binfasi. (Sun)

Crystal Palace, Leicester City na Middlesbrough ni miongoni mwa timu zilizo na hamu ya kumsajili beki wa kati wa Wolves Cameron John, mwenye miaka 20, ambaye anacheza kwa mkopo huko Doncaster Rovers. (Mail)iverpool inachunguza hali ya mchezaji mwenye umri wa miaka 20 raia wa Uholanzi Donyell Malen ambaye amefunga magoli 10 katika mechi 12 akiichezea PSV Eindhoven msimu huu (Calciomercato - in Italian)

Manchester United imeanzisha mazungumzo na kiungo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 20 Angel Gomes kuhusu mkataba mpya katika uwanja wa Old Trafford. (Manchester Evening News)

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy anasisitiza kwamba deni la £637m la ujenzi wa uwanja mpya halitakuwa na athari yoyote kuhusu dirisha la uhamisho la klabu hiyo... (Standard)