Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 21.09.2019: Alonso, Gomes, Wenger, Moutinho, Meunier

Xabi Alonso

Rais wa Real Madrid anamfikiria mchezaji wa zamani wa Liverpool na Uhispania Xabi Alonso kuchukua mahala pake Zinedine Zidane. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho pamoja na mkufunzi wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri pia wameorodheshwa kumrithi Zidane iwapo raia huyo wa Ufaransa atafutwa kazi. (Marca)

Wolves wamepiga hatua yao ya mazungumzo na mchezaji mwenye umri wa miaka 33 raia wa Ureno Joao Moutinho kuhusu kandarasi mpya ya miaka miwili katika uwanja wa Molineux. (Telegraph)

Watford inatumai kuipiku Hull katika usajili wa mshambuliaji wa Malmo na Sweden mwenye umri wa miaka 19 Kevin Harletun, ambaye atapatikana kwa dau la fidia ya £140,000 wakati kandarasi yake itakapokamilika Novemba. (Sun)

Massimiliano Allegri

Liverpool inachunguza hali ya mchezaji mwenye umri wa miaka 20 raia wa Uholanzi Donyell Malen ambaye amefunga magoli 10 katika mechi 12 akiichezea PSV Eindhoven msimu huu (Calciomercato - in Italian)

Manchester United imeanzisha mazungumzo na kiungo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 20 Angel Gomes kuhusu mkataba mpya katika uwanja wa Old Trafford. (Manchester Evening News)

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy anasisitiza kwamba deni la £637m la ujenzi wa uwanja mpya halitakuwa na athari yoyote kuhusu dirisha la uhamisho la klabu hiyo... (Standard)

Rais wa Real Madrid Florentino Perez na Jose Mourinho kulia

Newcastle ina hamu ya mchezaji mwenza wa Paraguay Miguel Almirons katika klabu ya Atlanta raia wa Venezuela Josef Martinez, 26. (Newcastle Chronicle)

Beki wa Ubelgiji Thomas Meunier amekiri kwamba anahisi kukerwa katika timu yake kufuatia kukosa muda wa kucheza katika timu ya PAG.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alihusishwa na kujiunga na Arsenal na Man United msimu huu. (RMC

Thomas Meunier

Mkufunzi wa Everton Marco Silva anasema kwamba klabu hiyo inafikiria uwezo wa kumsaini beki wa kati katika dirisha la uhamisho la mwezi. (Liverpool Echo)

Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger atachukua wadhfa wa kiufundi katika shirikisho la soka duniani Fifa katika kipindi cha wiki chache zijazo licha ya kuwa na hamu ya kuwa mkufunzi kwa mara nyengine.. (ESPN)

Aston Villa imetenga kitita cha £20m kununua mshambuliaji mpya mwezi Januari baada ya kuwakosa wachezaji iliokuwa ikiwalenga msimu. (Football Insider)

Mkufunzi wa zamani wa Real Madrid Santiago Solari anapigania kuwa mkufunzi wa kwanza wa klabu ya David Beckham Inter Miami. (BeINSports on Twitter)

Mkufunzi wa zamani wa Real Madrid Santiago Solari

Barcelona inahitaji kitita cha Yuro za au (£88m) baada ya mauzo ya wachezaji ili kuweka sawa matumizi ya kuafikia masharti ya Fifa ya fair Play. (Marca)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anataraji naibu wake na mchezaji wa zamani wa Everton Mikel Arteta atamrithi atakapoondoka. (Evening Standard)

Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 26, amewataka wachezaji wenzake kujiimarisha wakati ambapo klabu hiyo inaendelea kushuka kwa kiwango cha mchezo. (Sun)

Wilfried Zaha

Uwanja wa klabu ya Manchester City wa Etihad Stadium umeorodheshwa kuwa uwanja bora duniani na utafiti kuhusu timu zilizoshindia mataifa na maeneo yao, wakivishinda viwanja vya timu kama Barcelona- Nou Camp na Bayern Munich - Allianz Arena. (Mail)

TETESI ZA SOKA IJUMAA

Zidane

Chanzo cha picha, Getty Images

Klabu ya Real Madrid itawapasa watoe kitita cha euro milioni 80 wakitaka kumfuta kazi kocha wao Zinedine Zidane. Zidane amekuwa kwenye shinikizo kubwa kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri. (Sport)

Barcelona sasa ni klabu kubwa nyengine inayotajwa kumnyemelea mshambuliaji kinda Erling Braut Haaland, 19, wa klabu ya Red Bull Salzburg. Raia huyo wa Norway alikuwa mwiba mkali kwa klabu ya KRC Genk (inayochezewa na Mtanzania Mbwana Samatta) kwa kufumania nyavu zao mara tatu siku ya Jumanne. (Mundo Deportivo)

Baba wa Haaland, Alf-Inge, ameweka wazi kuwa itakuwa "vizuri" endapo mwanawe atajiunga na Manchester United, licha ya baba mtu kuchezea klabu hasimu za Leeds na Manchester City katika enzi zake. (TV2 kupitia Mail)

Klabu ya Liverpool imeanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba wa miaka mitano unusu mshambuliaji wake rai wa Senegal Sadio Mane, 27. Mkataba huo utamfanya Mane awe mchezaji anayelipwa vizuri zaidi Anfield kwa kitita cha pauni 220,000 kwa wiki. (Gazzetta dello Sport kupitia Star)

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Uhispania David Silva, 33, anatarajiwa kujiunga na klabu inayomilikiwa na David Beckham Inter Miami ya nchini Marekani pindi tu mkataba wake na Man City utakapofikia tamati mwishoni mwa msimu huu. (Independent)

Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku na mchezaji mwenza Marcelo Brozovic ilibidi waamuliwe na Alexis Sanchez baada ya kuibuka tafrani kwenye chumba cha kubadili nguo baada sare ya 1-1 Slavia Prague siku ya Jumanne. (Mail)

Lukaku

Chanzo cha picha, Reuters

Mmiliki wa klabu ya Arsenal Stan Kroenke alitoa pesa yake mfukoni kusajili wachezaji katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi badala ya kutegemea pesa kutoka kwenye vyanzo vya klabu kama inavyoinishwa kwenye sera zao.(Mirror)

Chelsea wana Imani kuwa majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata kiungo wao Mason Mount, 20, kwenye mchezo dhidi ya Valencia siku ya Jumanne si makubwa kama ilivyohofiwa hapo awali. (Standard)

Leicester wametuma maskauti wao kumtazama beki wa pembeni wa Benfica, Mreno Andre Almeida, 29, kwenye mchezo dhidi ya RB Leipzig siku ya Jumanne. (Record kupitia Leicester Mercury)

Kiungo wa Switzerland Xherdan Shaqiri, 27, amesema anahisi "kutokuwa na furaha kidogo" kwa kupata muda mdogo wa kucheza klabuni Liverpool msimu huu japo anasisitiza kuwa yungali na "furaha" kuwa Anfield. (Liverpool Echo)

Everton na Newcastle wamekuwa wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya mshambuliaji wa Atlanta United na Venezuela Martinez, 25. (Chronicle)

Kiungo wa Aston Villa Jack Grealish, 24, anaamini kuwa anaweza kuchezea timu ya taifa ya England baada ya kupewa maneno ya hamasa na kocha msaidiza wa Villa John Terry. (Standard)

Tetesi za Alhamisi

POGBA

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United inatumai kumshawishi mchezaji wa kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 26 Paul Pogba kusaini mkataba mpya. Mchezaji wa kiungo cha kati wa England Jesse Lingard, mwenye umri wa miaka 26, na mchezaji wa kiungo cha mbele wa miaka 17 anayeichezea timu ya taifa ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Mason Greenwood pia wameorodheshwa kwa mikataba mipya. (Standard)

Mashabiki wenye hasira wa Real Madrid wametaka Zinedine Zidane afutwe kazi kama meneja wa timu hyo baada ya Paris St-Germain kuitandika kichapo katika mechi ya ligi ya mabingwa (Sun)

Juventus imekataa fursa ya kumsajili Dani Alves msimu huu wa joto kabla ya mlinzi huyo mwenye miaka 36 kujiunga na Sao Paulo katika uhamisho wa bure. (Calciomercato)

Manchester United imetuma wakala kwenda kumtazama mchezaji wa kiungo cha mbele wa Norway Erling Haaland, mwenye umri wa miaka 19, wakati akijitambulisha katika jukwa la Ulaya kwa kuifungia Red Bull Salzburg katika mechi yake ya kwanza katika ligi ya mabingwa . (Salzburger Nachrichten, kupitia Sport Witness)

Blackburn inafanya mazungumzo kumsajili aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham na Fulham Lewis Holtby, raia huyo wa Ujerumani mwenye miaka 29 ambaye amekuwa wakala wa bure tangu aondoke Hamburg msimu uliopita. (Mail)

LEWIS HOLTBY

Chanzo cha picha, Getty Images

Everton ina hamu ya kumsajili mshambuliaji mwenye umri wamiaka 19 wa Ireland kaskazini David Parkhouse, ambaye kwa sasa amechukuliwa kwa mkopo na Derry City kutoka Sheffield United. (Football Insider)

Kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer, mwenye umri wa miaka 33, anafikiria kustaafu kutoka soka ya kimataifa na Ujerumani baada ya mashindano ya ubingwa mwaka ujao. (Bild)

Winga wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 19 Jadon Sancho, anayelengwa na Manchester United amekataa kuthibitisha kutoondoka kutoka klabu hiyo msimu ujao wa majira ya joto. (Viasport, kupitia Metro)

Manchester United inaiangalia hali ya Thomas Tuchel akiwa huko Paris St-Germain iwapo wataamua kuijaza nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer. (Le10 Sport, kupitia Sport Witness)

Mlinzi Virgil van Dijk, mwenye miaka 28, amepuuzia pendekezo kuwa anakaribia kukubali mkataba mpya na Liverpool. (Sky Sports, kupitia Mail)

Virgil van Dijk,

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea imefungua mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha mbele Tammy Abraham na mlinzi Fikayo Tomori kuwapatia wachezaji hao wa timu ya taifa ya England mikataba ya miaka mitano kila mmoja. (Guardian)

Tottenham inafikiria iwapo kumrudisha winga Jack Clarke kutoka uhamisho wake wa mkopo huko Leeds huku mchezaji huyo wa miaka 19 akitarajiwa kushiriki mechi ya ligi msimu huu. (Mail)

Uefa itathibitisha uga wa Wembley kuwa mwenyeji wa mashindano ya fainali ya ligi ya mabingwa 2023 wiki ijayo. (Sky Sports)