Norwich City yaweka historia kwa kuilaza Man City 3-2

Norwich yailaza Man City

Chanzo cha picha, Reuters

Klabu ya Norwich City iliopanda daraja na kujiunga na ligi ya Uingereza ya Premia imeweka historia baada ya kuwalaxza mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester City .

Norwich ilisitisha msururu wa Man City kucheza timu 18 bila kushindwa katika mechi ya kusisimua.

Shambulio la Kenny Mclean kutoka katika kona liliwaweka kifua mbele wachezaji hao wa canary baada ya dakika ya 18 kabla ya kuongeza uongozi wao baada ya dakika 30 wakati walipovamia lango la Man City huku mchezaji Todd Cantewel akifunga

Sergio Aguero alipunguza uongozi huo wa Norwich kupitia bao la kichwa kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika lakini Teemu Pukki alichukua fursa ya masikhara ya Nicolas Otamendi mapema katika kipindi cha pili kuongeza idadi hiyo ya mabao.

Hatahivyo Shambulio la Rodri karibu na eneo hatari ikiwa imesalia dakika mbili liliipatia City matumaini , lakini Norwich ilihimili kishinda cha mashambulizi ya Man City na kupata ushindi wao wa pili msimu huu.

Klabu hiyo ya Daniel Farke iliondoka katika mkia wa jedwali la ligi ya EPL na kupanda hadi nafasi ya 12 huku City ikisalia katika nafasi ya pili lakini wakiwa pointi tano nyuma wa viongozi wa ligi Liverpool.

Matokeo mengine ya EPL

Matokeo mengine ya EPL