Taifa gani lingeshinda taji la Afcon kwa mambo mengine kando na soka?

Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yanaendelea nchini Misri huku timu 24 zikiminyana kwa mara ya kwanza. Lakini nje ya uwanja, tunafikiri kuwa ni jambo la kufurahisha kuuliza: "Je wajua nani atashinda mataji mengine ukiacha la mpira linaloshindaniwa AFCON?" Katika mchezo wetu tunazigonganisha nchi mbalimbali ili kupata bingwa kwenye kasi ya intaneti, umri wa kuishi, rushwa na mambo mengine.
Chagua kundi
News image
  • Nchi gani ina kasi zaidi ya intaneti?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • Zimbabwe vs Kenya. Msindi: Kenya
        • Afrika Kusini vs Tunisia. Msindi: Afrika Kusini
        • Madagascar vs Cote d'Ivoire. Msindi: Madagascar
        • Ghana vs Mali. Msindi: Ghana
        • Angola vs Morocco. Msindi: Morocco
        • Senegal vs DR Congo. Msindi: Senegal
        • Nigeria vs Kameruni. Msindi: Nigeria
        • Uganda vs Tanzania. Msindi: Uganda
    • Robo Fainali
        • Kenya vs Afrika Kusini. Msindi: Afrika Kusini
        • Madagascar vs Ghana. Msindi: Madagascar
        • Morocco vs Senegal. Msindi: Senegal
        • Nigeria vs Uganda. Msindi: Uganda
    • Nusu Fainali
        • Afrika Kusini vs Madagascar. Msindi: Madagascar
        • Senegal vs Uganda. Msindi: Senegal
    • Fainali
        • Madagascar
          Senegal
          Madagascar vs Senegal. Msindi: Madagascar
    News imageNews image
    Madagascar
    Mwezi Mei 2019, kasi ya intaneti nchini Madagascar ilikuwa 28.08 megabits kwa sekunde - hiyo ni kasi ya pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya ile ya Cape Verde. Lakini kasi hiyo, haimaanishi kuwa watu wengi wanatumia intaneti. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mwaka 2017 ni asilimia 10 tu ya wananchi wa Madagascar ndio walikuwa wakitumia intaneti
    Chanzo: Speetest Global Index by Ookla. Download speed for fixed broadband, May 2019. Data for Guinea-Bissau and Guinea unavailable.
    News image
  • Nchi gani inakula zaidi wali?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • Uganda vs Tanzania. Msindi: Tanzania
        • Cote d'Ivoire vs Ghana. Msindi: Cote d'Ivoire
        • Guinea vs Kenya. Msindi: Guinea
        • Guinea-Bissau vs Mauritania. Msindi: Guinea-Bissau
        • Mali vs Afrika Kusini. Msindi: Mali
        • Senegal vs Nigeria. Msindi: Senegal
        • Madagascar vs Benin. Msindi: Madagascar
        • Misri vs Angola. Msindi: Misri
    • Robo Fainali
        • Tanzania vs Cote d'Ivoire. Msindi: Cote d'Ivoire
        • Guinea vs Guinea-Bissau. Msindi: Guinea
        • Mali vs Senegal. Msindi: Senegal
        • Madagascar vs Misri. Msindi: Madagascar
    • Nusu Fainali
        • Cote d'Ivoire vs Guinea. Msindi: Guinea
        • Senegal vs Madagascar. Msindi: Senegal
    • Fainali
        • Guinea
          Senegal
          Guinea vs Senegal. Msindi: Guinea
    News imageNews image
    Guinea
    Mwaka 2018, inakisiwa kila raia Guinea kwa wastani alikula kilo 190 ya mchele. Japo wana hali ya hewa nzuri kwa kulima mpunga, mchele ndiyo bidhaa inayoagizwa kwa wingi kutoka nje. Wanaagiza zaidi kutoka bara Asia.
    Chanzo: IRRI. Estimated milled rice consumption per capita, 2018. No data for Benin, Namibia, Tunisia and Zimbabwe
    News image
  • Nchi gani ina Pato la Taifa (GDP) kubwa?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • Zimbabwe vs Kenya. Msindi: Kenya
        • Afrika Kusini vs Mauritania. Msindi: Afrika Kusini
        • Nigeria vs Morocco. Msindi: Morocco
        • Ghana vs Tunisia. Msindi: Tunisia
        • Angola vs Namibia. Msindi: Namibia
        • Algeria vs Benin. Msindi: Algeria
        • Guinea vs Kameruni. Msindi: Kameruni
        • Misri vs Senegal. Msindi: Senegal
    • Robo Fainali
        • Kenya vs Afrika Kusini. Msindi: Afrika Kusini
        • Morocco vs Tunisia. Msindi: Tunisia
        • Namibia vs Algeria. Msindi: Namibia
        • Kameruni vs Misri. Msindi: Misri
    • Nusu Fainali
        • Afrika Kusini vs Tunisia. Msindi: Afrika Kusini
        • Namibia vs Misri. Msindi: Namibia
    • Fainali
        • Afrika Kusini
          Namibia
          Afrika Kusini vs Namibia. Msindi: Afrika Kusini
    News imageNews image
    Afrika Kusini
    Wastani wa pato la mtu nchini Afrika Kusini ni zaidi ya dola 6,000 kwa mwaka, kwa mujibu wa Benki ya Dunia. Lakini Afrika ya Kusini inasalia kuwa ni moja ya nchi yenye uchumi usio na uwiano duniani. Japo nchi hiyo ina watu wengi zaidi wenye uwezo wa kifedha barani Afrika, ukosefu wa ajira nchini humo kwa miezi minne ya mwisho ya 2018 ulikuwa ni wastani wa asilimia 27. Hali ya umasikini ni kubwa nchini humo.
    Chanzo: World Bank, GDP per capita, Current US$, 2017
    News image
  • Nchi gani ina deni dogo la taifa?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • Misri vs Tanzania. Msindi: Tanzania
        • Cote d'Ivoire vs Benin. Msindi: Benin
        • Nigeria vs Uganda. Msindi: Nigeria
        • Guinea-Bissau vs Angola. Msindi: Guinea-Bissau
        • Mali vs Morocco. Msindi: Mali
        • Algeria vs Burundi. Msindi: Algeria
        • Guinea vs Kameruni. Msindi: Guinea
        • DR Congo vs Kenya. Msindi: DR Congo
    • Robo Fainali
        • Tanzania vs Benin. Msindi: Benin
        • Nigeria vs Guinea-Bissau. Msindi: Nigeria
        • Mali vs Algeria. Msindi: Algeria
        • Guinea vs DR Congo. Msindi: DR Congo
    • Nusu Fainali
        • Benin vs Nigeria. Msindi: Nigeria
        • Algeria vs DR Congo. Msindi: Algeria
    • Fainali
        • Nigeria
          Algeria
          Nigeria vs Algeria. Msindi: Algeria
    News imageNews image
    Algeria
    Mapato makubwa yatokanayo na mafuta na matumizi mazuri ya hifadhi ya pesa zinazotokana na mafuta imeviwezesha Algeria kukuaribia kulifuta kabisa deni lao la nje mpaka kufikia 3.4% ya pato la taifa. Hiyo ina maana kuwa endapo raia wa nchi hiyo wataamua kutoa mishahara yao, itawachukua siku 12 tu kulipa deni hilo lililosalia. Nchini Mauritania itawachukua siku 311 kufanya hivyo.
    Chanzo: World Bank (IDS), Total External Debt to GNI (%), 2017. No data for Namibia.
    News image
  • Nchi gani watu wake wanaishi muda mrefu zaidi?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • Uganda vs Senegal. Msindi: Senegal
        • Morocco vs Angola. Msindi: Morocco
        • Nigeria vs Afrika Kusini. Msindi: Afrika Kusini
        • Ghana vs Mauritania. Msindi: Mauritania
        • Tunisia vs Namibia. Msindi: Tunisia
        • Algeria vs Kameruni. Msindi: Algeria
        • Madagascar vs Benin. Msindi: Benin
        • Misri vs Tanzania. Msindi: Misri
    • Robo Fainali
        • Senegal vs Morocco. Msindi: Morocco
        • Afrika Kusini vs Mauritania. Msindi: Mauritania
        • Tunisia vs Algeria. Msindi: Tunisia
        • Benin vs Misri. Msindi: Misri
    • Nusu Fainali
        • Morocco vs Mauritania. Msindi: Morocco
        • Tunisia vs Misri. Msindi: Tunisia
    • Fainali
        • Morocco
          Tunisia
          Morocco vs Tunisia. Msindi: Tunisia
    News imageNews image
    Tunisia
    Raia wa Tunisia waliozaliwa 2017 wanategemea kuishi mpaka kufikia miaka 78, kati ya hiyo 67 wakiwa na afya njema. Wanawake wanatarajiwa kufikia miaka 80 na wanaume 76. Vyanzo vikuu vya vifo vya mapema nchini humo ni magonjwa ya moyo na ajali za barabarani.
    Chanzo: Global Burden of Disease Study 2017, Institute for Health Metrics and Evaluation.
    News image
  • Nchi gani ina watu wengi zaidi?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • DR Congo vs Kenya. Msindi: DR Congo
        • Afrika Kusini vs Guinea. Msindi: Afrika Kusini
        • Nigeria vs Cote d'Ivoire. Msindi: Nigeria
        • Ghana vs Mali. Msindi: Ghana
        • Angola vs Morocco. Msindi: Morocco
        • Tanzania vs Uganda. Msindi: Tanzania
        • Madagascar vs Kameruni. Msindi: Madagascar
        • Misri vs Algeria. Msindi: Misri
    • Robo Fainali
        • DR Congo vs Afrika Kusini. Msindi: DR Congo
        • Nigeria vs Ghana. Msindi: Nigeria
        • Morocco vs Tanzania. Msindi: Tanzania
        • Madagascar vs Misri. Msindi: Misri
    • Nusu Fainali
        • DR Congo vs Nigeria. Msindi: Nigeria
        • Tanzania vs Misri. Msindi: Misri
    • Fainali
        • Nigeria
          Misri
          Nigeria vs Misri. Msindi: Nigeria
    News imageNews image
    Nigeria
    Ikiwa na zaidi ya watu milioni 200, Nigeria ndio nchi yenye watu wengi zaidi Afrika na ya 7 duniani. Pia watu wa taifa hilo wana umri mdogo, wat wanne kati ya 10 wapo chini ya miaka 14.
    Chanzo: CIA World Factbook, estimated population in 2018
    News image
  • Nchi gani ina eneo kubwa zaidi?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • Misri vs Tanzania. Msindi: Misri
        • Afrika Kusini vs Mauritania. Msindi: Afrika Kusini
        • Nigeria vs Morocco. Msindi: Nigeria
        • Kameruni vs Mali. Msindi: Mali
        • Angola vs Namibia. Msindi: Angola
        • Algeria vs Zimbabwe. Msindi: Algeria
        • Madagascar vs Ghana. Msindi: Madagascar
        • DR Congo vs Kenya. Msindi: DR Congo
    • Robo Fainali
        • Misri vs Afrika Kusini. Msindi: Afrika Kusini
        • Nigeria vs Mali. Msindi: Nigeria
        • Angola vs Algeria. Msindi: Algeria
        • Madagascar vs DR Congo. Msindi: DR Congo
    • Nusu Fainali
        • Afrika Kusini vs Mali. Msindi: Mali
        • Algeria vs DR Congo. Msindi: Algeria
    • Fainali
        • Mali
          Algeria
          Mali vs Algeria. Msindi: Algeria
    News imageNews image
    Algeria
    Algeria ndio nchi kubwa zaidi Afrika na ya 10 duniani. Hata hivyo zaidi ya 80% ya eneo lake ni jangwa la Sahara. Nchi kubwa zaidi ilikuwa ni Sudani, kabla ya kugawanyika mwaka 2011. Algeria haina msongamano mkubwa wa watu, kwa kilometa mraba moja kuna watu 17 wakati Burundi ina watu 423 kwa eneo la ukubwa kama huo.
    Chanzo: World Bank, 2018
    News image
  • Nchi gani yenye kiwango kidogo cha rushwa?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • Uganda vs Tanzania. Msindi: Tanzania
        • Namibia vs Mauritania. Msindi: Namibia
        • Guinea vs Morocco. Msindi: Morocco
        • Ghana vs Mali. Msindi: Ghana
        • Tunisia vs Afrika Kusini. Msindi: Afrika Kusini
        • Senegal vs Kameruni. Msindi: Senegal
        • Nigeria vs Benin. Msindi: Benin
        • Misri vs Algeria. Msindi: Algeria
    • Robo Fainali
        • Tanzania vs Namibia. Msindi: Namibia
        • Morocco vs Ghana. Msindi: Morocco
        • Afrika Kusini vs Senegal. Msindi: Senegal
        • Benin vs Algeria. Msindi: Benin
    • Nusu Fainali
        • Namibia vs Morocco. Msindi: Namibia
        • Senegal vs Benin. Msindi: Senegal
    • Fainali
        • Namibia
          Senegal
          Namibia vs Senegal. Msindi: Namibia
    News imageNews image
    Namibia
    Namibia ndiyo nchi inayotajwa kuwa na kiwango kidogo cha rushwa kwenye nchi zinazochuana kwenye AFCON, ikiishinda hata Senegal. Kwa mujibu wa ripoti ya dunia ya rushwa ya 2018, ipo nafasi ya tano Afrika, ambapo kinara ni Ushelisheli. Duniani, Namibia inazishinda nchi kama Italia na Uturuki.
    Chanzo: Corruption Perception Index, 2018. Transparency International
    News image
  • Nchi gani raia wake wana furaha?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • Uganda vs Senegal. Msindi: Senegal
        • Morocco vs Mali. Msindi: Morocco
        • Nigeria vs Afrika Kusini. Msindi: Nigeria
        • Kameruni vs Tunisia. Msindi: Kameruni
        • Mauritania vs Cote d'Ivoire. Msindi: Cote d'Ivoire
        • Algeria vs Benin. Msindi: Algeria
        • Guinea vs Ghana. Msindi: Ghana
        • DR Congo vs Kenya. Msindi: Kenya
    • Robo Fainali
        • Senegal vs Morocco. Msindi: Morocco
        • Nigeria vs Kameruni. Msindi: Nigeria
        • Cote d'Ivoire vs Algeria. Msindi: Algeria
        • Ghana vs Kenya. Msindi: Ghana
    • Nusu Fainali
        • Morocco vs Nigeria. Msindi: Nigeria
        • Algeria vs Ghana. Msindi: Algeria
    • Fainali
        • Nigeria
          Algeria
          Nigeria vs Algeria. Msindi: Nigeria
    News imageNews image
    Nigeria
    Nigeria inaongoza kwa wale wote walio AFCON kwa mujibu wa ripoti ya 2019, ambayo huangalia vitu kama kipato, afya, kutokuwepo kwa rushwa, uungwana na uhuru. Duniani Nigeria ipo katika nafasi ya 85, mwaka jana walikuwa nafasi ya 91. Kwa Afrika ni nchi ya pili nyuma ya Mauritius.
    Chanzo: World Happiness Report 2019.
    News image
  • Nchi gani ina wanawake wengi bungeni?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • Zimbabwe vs Tanzania. Msindi: Tanzania
        • Namibia vs Mauritania. Msindi: Namibia
        • Burundi vs Morocco. Msindi: Burundi
        • Angola vs Kameruni. Msindi: Angola
        • Tunisia vs Afrika Kusini. Msindi: Afrika Kusini
        • Senegal vs Madagascar. Msindi: Senegal
        • Guinea vs Guinea-Bissau. Msindi: Guinea
        • Uganda vs Algeria. Msindi: Uganda
    • Robo Fainali
        • Tanzania vs Namibia. Msindi: Namibia
        • Burundi vs Kameruni. Msindi: Burundi
        • Afrika Kusini vs Senegal. Msindi: Afrika Kusini
        • Guinea vs Uganda. Msindi: Uganda
    • Nusu Fainali
        • Namibia vs Burundi. Msindi: Namibia
        • Afrika Kusini vs Uganda. Msindi: Afrika Kusini
    • Fainali
        • Namibia
          Afrika Kusini
          Namibia vs Afrika Kusini. Msindi: Namibia
    News imageNews image
    Namibia
    Namibia wanawake ni asilimia 46 bungeni. Nchi hiyo ipo nyuma ya Rwanda tu, ambayo ndio kinara duniani katika eneo hilo. Namibia pia ipo nafasi ya 10 duniani kwa pengo dogo la kipato baina ya wanawake na wanaume ikiwashinda mpaka Ujerumani na Uingereza.
    Chanzo: Inter-Parliamentary Union
    News image
  • Nchi gani imeshinda medali nyingi za Olimpiki?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • Zimbabwe vs Algeria. Msindi: Algeria
        • Afrika Kusini vs Madagascar. Msindi: Afrika Kusini
        • Nigeria vs Cote d'Ivoire. Msindi: Nigeria
        • Kameruni vs Angola. Msindi: Kameruni
        • Tunisia vs Morocco. Msindi: Morocco
        • Kenya vs Uganda. Msindi: Kenya
        • Burundi vs Ghana. Msindi: Burundi
        • Misri vs Tanzania. Msindi: Misri
    • Robo Fainali
        • Algeria vs Afrika Kusini. Msindi: Afrika Kusini
        • Nigeria vs Kameruni. Msindi: Nigeria
        • Morocco vs Kenya. Msindi: Kenya
        • Burundi vs Misri. Msindi: Misri
    • Nusu Fainali
        • Afrika Kusini vs Nigeria. Msindi: Afrika Kusini
        • Kenya vs Misri. Msindi: Kenya
    • Fainali
        • Afrika Kusini
          Kenya
          Afrika Kusini vs Kenya. Msindi: Kenya
    News imageNews image
    Kenya
    Kenya ndio bingwa katika eneo hilo, medali za dhahabu 31, fedha 38, na shaba 34. Kenya imeshinda medali nyingi katika eneo la riadha, hasa mbio ndefu.
    Chanzo: IOC
    News image
  • Nchi gani ina maeneo mengi ya Hifadhi ya Urithi wa Dunia?
    • Mzunguko wa 16 bora
        • DR Congo vs Senegal. Msindi: Senegal
        • Afrika Kusini vs Benin. Msindi: Afrika Kusini
        • Madagascar vs Cote d'Ivoire. Msindi: Cote d'Ivoire
        • Kameruni vs Mali. Msindi: Mali
        • Tunisia vs Morocco. Msindi: Morocco
        • Kenya vs Zimbabwe. Msindi: Kenya
        • Nigeria vs Ghana. Msindi: Nigeria
        • Misri vs Algeria. Msindi: Misri
    • Robo Fainali
        • Senegal vs Afrika Kusini. Msindi: Afrika Kusini
        • Cote d'Ivoire vs Mali. Msindi: Mali
        • Morocco vs Kenya. Msindi: Morocco
        • Nigeria vs Misri. Msindi: Misri
    • Nusu Fainali
        • Afrika Kusini vs Mali. Msindi: Afrika Kusini
        • Morocco vs Misri. Msindi: Morocco
    • Fainali
        • Afrika Kusini
          Morocco
          Afrika Kusini vs Morocco. Msindi: Afrika Kusini
    News imageNews image
    Afrika Kusini
    Afrika Kusini ina maeneo 10, ikiwemo ya binadamu wa kale na kisiwa cha Robben ambacho Nelson Mandela alifungwa.
    Chanzo: UNESCO.
    News image
    • Afrika Kusini
    • Algeria
    • Angola
    • Benin
    • Burundi
    • Cote d'Ivoire
    • DR Congo
    • Ghana
    • Guinea
    • Guinea-Bissau
    • Kameruni
    • Kenya
    • Madagascar
    • Mali
    • Mauritania
    • Misri
    • Morocco
    • Namibia
    • Nigeria
    • Senegal
    • Tanzania
    • Tunisia
    • Uganda
    • Zimbabwe
Imeandaliwa na Olawale Malomo na Elisabetta Tollardo, Olawale Malomo, Millicent Wachira, Aaron Akinyemi, Anthony Makokha na Muthoni Muchiri.
Methodolojia
Nchi zinazoshiriki AFCON zimeorodheshwa kulingana na kiwango katika maeneo 12, ambayo ipo juu ndio mshindi. Nchi zinashindanishwa kama ilivyo kwenye ratiba rasmi ya mashindan yanayoendelea Misri. Tofauti ipo katika maeneo mawili ambayo ni medali za olimpiki na Maeneo ya Hifadhi ya Urithi wa Dunia. Kwenye upande wa medali,nchi zimeorodheshwa kulingana na medali za dhahabu, fedha na shaba.

.