Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 29.06.2019: Pogba, Zaha, Aubameyang, Lampard, Falcao, Camacho

Auba

Chanzo cha picha, Reuters

Arsenal wapo tayari kumuuza mshambuliaji wao raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, lakini si kwa Manchester United ama Liverpool. (90min.com)

Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, ameiomba klabu yake ya Crystal Palace imruhusu ahamie Arsenal. Palace inamthaminisha streka huyo streka huyo kuwa na thamani ya pauni milioni 80. (Mirror)

Manchester United wanamini kuwa wataweza kukamilisha usajili wa kuwanasa Sean Longstaff, 21, kutoka Newcastle na Bruno Fernandes, 24, kutoka Sporting Lisbon ya Ureno. (Evening Standard)

Real Madrid watalazimika kulipa kitita cha pauni milioni 150 ili kumsajili kiungo Mfaransa Paul Pogba 26, kutoka Manchester United. (Mirror)

Pogba

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Pogba

Gareth Bale yawezekana akasilia na Real Madrid baada ya klabu hiyo kushindwa kumpata mnunuzi anayemtaka winga huyo mwenye miaka 29. (Mirror)

Chelsea wanampango wa kumtangaza Frank Lampard kuwa kocha wao mpya kabla ya wachezaji kurudi mpaumzikoni wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao. plan to announce Derby. (Sun)

Frank Lampard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lampard ni moja kati ya wachezaji waloichezea Chelsea kwa mafanikio makaubwa

Liverpool wamefikia makubaliano na Sporting ada ya usajili ipatayo pauni milioni 7 ili kumnunua mshambuliaji kinda Rafael Camacho, 19. (Evening Standard)

Kumefanyika mkutano baina ya viongozi wakuu wa Atletico na Real Madrid juu ya usajili wa usajili wa mshambuliaji Antoine Griezmann, 28, kuelekea dimba la Bernabeu. (L'Equipe - in French)

Antoine Griezmann
Maelezo ya picha, Antoine Griezmann kutimkia Barcelona ama Atlit

Streka wa Colombia Radamel Falcao, 33, anataka kujiunga na timu inayomilikiwa na David Beckham nchini Marekani Miami pale mkataba wake watakapofiki tamati na klabu ya Monaco. (Sun)

Aston Villa wapo tayari kutuma maombi ya kutaka kumsajili beki wa Southampton Matt Targett. (Express and Star)

Kocha wa West Brom Slaven Bilic anamtaka mchezaji mwenzake wa zamani klabuni hapo Julian Dicks kujiunga naye kama sehemu ya benchi la ufundi.. (Express and Star)

Tetesi bora za Ijumaa

Umtiti

Manchester United inafikiria kumnunua beki wa Ufaransa na Barcelona Samuel Umtiti, 25. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mshambuliaji wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 23, anasalia kuwa mchezaji anayelengwa sana na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich msimu huu licha ya mpango huo kusita hapo awali. (Sky Sports)

Mkufunzi wa klabu ya Sporting Marcel Keizer anaamini kwamba nafasi ya kumzuia kiungo wa kati wa Portugal Bruno Fernandez katika klabu hiyo ni ndogo, huku Manchester United ikiwa miongoni mwa klabu ambazo zimevutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 (Record, via Manchester Evening News)

Kane

Chanzo cha picha, Getty Images

Babake mshambuliaji wa Juventus Moise Kean, 19, ametangaza kwamba raia huyo wa Italia anataka kuhamia Inter Milan. (Mirror)

Atletico Madrid inafikiria kumsajili mchezaji wa Real Madrid na Colombian James Rodriguez, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akiwa hahitajiki tena Real . (Cadena SER, via AS)

James Rodrigues

Naibu mkufunzi wa Chelsea Gianfranco Zola ataondoka Chelsea wikendi hii wakati ambapo kandarasi yake itakuwa inakamilika baada ya kukataa ofa ya kuwa balozi wa klabu hiyo. (Guardian)