Afcon 2019: Uganda yazuiliwa na Zimbabwe huku Misri ikiilaza DR Congo ili ikisonga mbele

Mohamed Salah

Chanzo cha picha, AFP

Uganda na Zimbabwe zilitoka sare ya moja kwa moja katika mechi ya kundi A la kinyanganyiro cha kombe la mataifa ya Afrika kinachoendelea nchini Misri.

Uganda ilichukua uongozi wa mapema kupitia Emmanuel Okwi baada ya mlinda lango wa Zimbabwe George Chigova kupangua shambulio la Lumala Abdi.

Lakini Zimbabwe ilisawazisha wakati Khama Billiat alipofunga baada ya kazi nzuri katika wingi ya kushoto iliofanywa na mchezaji Ovidy Karuru.

Wakati huohuo Nyota wa Misri Mohamed Salah alifunga bao moja na kutoa pasi iliosababisha kufungwa kwa bao la pili dhidi ya DR Congo na hivyobasi kuvuzu katika raundi ya muondoano ya timu 16.

Misri ilitangulia kufunga baada ya Salah kupigiwa pasi ya 'pesa' na mchezaji wa klabu ya Aston Villa Ahmed Elmohamady ambaye alifunga goli la pili.

Alifunga wakati mshambuliaji huyo wa Liverpool alipozungukwa na wachezaji wawili wa DR Congo baada ya mshambuliaji Trezeguet kumfanyia kazi nzuri.

Misri ambao ni mabingwa mara saba wa kombe hilo wanajiunga na Nigeria katika mechi za muondoano.

Guinea ikimenyana na Nigeria

Chanzo cha picha, Reuters

Nigeria iliwalaza Guinea kwa bao moja kwa nunge katika mechi ya ufunguzi siku ya Jumatano ili kuwa taifa la kwanza kufuzu katika raundi ya muondoano.

Uganda ilitoka sare na Zimbabwe

Chanzo cha picha, Reuters

Wakati huohuo mchezaji wa Zimbabwe Knowledge Musona na mchezaji wa Uganda Patrick Kadu wote walikosa fursa nzuri ya kufunga goli.

Musona aligonga mwamba wa goli wakati aliposalia maguu manne na goli baada ya shambulizi la mchezaji wa Zimbabwe Evans Rusike kuokolewa lilipokuwa likikaribia mstari wa goli, Kaddu aliupiga mpra huo nje.

Zimbabwe ambao walikuwa wanalenga kupata ushindi wao wa tatu katika michuano ya Afcon sasa watalazimika kuishinda DR Congo katika mechi yao ya mwisho ya kundi lao siku ya Jumapili ili kuweza kupata nafasi ya kufuzu katika raundi ya muondoano kwa mara ya kwanza.