Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Pogba, Klopp, Bowen, Hazard, Alderweireld, Bielsa, Icardi

Chanzo cha picha, Reuters
Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25, amebadilisha mpango wa kuondoka Old Trafford msimu wa joto baada ya kufanya mazungumzo na meneja wa muda wa klabu hiyo Ole Gunnar Solksjaer. (Sun)
Mpango wa United wa kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Ivan Rakitic, 31 umefififa. (Evening Standard)
Rais wa zamani wa Bayern Munich, Franz Beckenbauer amemuunga mkono meneja wa sasa wa Liverpool Jurgen Klopp kuwaongoza klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama, Bundesliga. (Goal)
Kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard "hajawahi kusema lolote kuhusu Real Madrid", kwa mujibu wa mchezaji mwenzake Willian.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nyota huyo wa miaka 26 raia wa Ubelgiji amehusishwa na tetesi ya kuhamia klabu ya La Liga. (Mail)
Mchezaji wa Hull City Jarrod Bowen amekataa ofa ya euro milioni 12 kuhamia Cardiff City baada ya klabu hiyo kujaribu kumsaini wakati Emiliano Sala alipopotea katika mkasa wa ndege, lakini hajathibitishwa kuwa amefariki.
Mchezaji huyo anasema hali hiyo 'ilikuwa ngumu sana". (Mail)
Juventus na Real Madrid zinatazamiwa kuwa vilabu ambavyo mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icardi huanda akajiunga navyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji huyo wa miaka 26 hajashiriki mashindano yenye ushindani mkubwa tangu alipovuliwa nafasi ya unahodha mwezi Februari. (TyC Sports, via Calciomercato)
Manchester United imepewa ishara ya wazi ya kumsajili mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld.
Kifungu cha sheria katika kandarasi ya kiungo huyo wa miaka 30 huenda kikamruhusu kuhama kwa kima cha euro milioni 26 msimu wa joto. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Rafael Benitez atalazimika kuwasajili wachezaji wadogo akiridhia kusaini mkataba mpya na Newcastle. (Mirror)
Real Madrid huenda akaibwaga Manchester United katika kinyang'anyiro cha usajili wa mlinzi wa Porto, Eder Militao. (Sun)
Meneja wa Leeds United Marcelo Bielsa huenda akaondoka uwanja wa Elland Road ikiwa klabu hiyo haitafuzu kujiunga na ligi ya Primia, kwa mujibu wa mlinzi wa zamani wa klabu hiyo Danny Mills. (Talksport)
Tetesi Bora Jumatano
Manchester United inatarajiwa kumsajili winga wa Borussia Dortmund muingereza Jadon Sancho.

Chanzo cha picha, Reuters
Klabu hiyo ya ligi ya primia pia imewasiliana na Barcelona kuhusiana na uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 28. (Independent)
Huku hayo yakijiri meneja wa muda wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer anajiandaa kuwapatia walinzi wake nafasi ya kujidhihirisha kuwa wanaweza kufikia matarajio yake kabla ya uamuzi kutolewa wa kumnunua beki wa kati kwa kima cha £80m msimu huu wa joto. (Sun)













