Lukaku ni 'mambo yote' asema Solskjaer

Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku

Chanzo cha picha, Reuters

Romelu Lukaku ana jukumu kubwa katika kikosi cha Manchester United, asema meneja wa muda wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer.

Lukaku ameanza mechi mara moja tangu Jose Mourinho afutwe kazi kama meneja wa klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Everton aliyejiunga na Man Utd kwa kima cha pauni milioni 75 amecheza mechi sita za ligi kuu ya England chini ya uongozi wa Solskjaer.

Solskjaer amesifia umahiri wa Rashford, Jesse Lingard na Anthony Martial.

Lakini raia huyo raia huyo wa Norway amesema Lukaku, 25, anasali kuwa "kiungo mhimu wa kikosi chake".

Ni Rashford na Paul Pogba ambao wamefunga zaidi ya mabao matatu yaliyotiwa kimyani na Lukaku tangu Mourinho alipotimuliwa Disemaba 18 mwaka jana

Romelu Lukaku alifungia Manchester United bao wwakati wa maechi yao dhidi ya Newcastle United Januari 2

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Romelu Lukaku amefunga mabao 36 katika mechi 77 aliyochezea Manchester United

Huku Alexis Sanchez na Juan Mata wakijikakamua kushirikishwa katika kikosi cha kwanza cha United, Solskjaer amejipata katika hali ambayo inamkumbusha enzi zake alipokua mchezaji wa Mashetani wekundu.

Alipohamia uwanja wa Old Trafford mwaka 1996, Solskjaer alifungia United jumla ya mabao 126 katika misimu 11.

Alisema: "Nilikua mmoja wa washambuliaji wanne wakati ni waliocheza walikua wawili. Sasa washambuliaji ni sita na wanaocheza ni watatu.

"Kuna michezo ya kutosha. Inategemea jinsi utakavyotumia nafasi yako .

"Hakuna mtu anaue funga mabao mengi kumshinda Romelu akiwa mazoezini."