Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 01.01.2019: Ozil, Ramsey, Pogba, Heaton, Hudson-Odoi, Rabiot

Pogba akicheza kusherehekea bao lake la kwanza mechi dhidi ya AFC Bournemouth ambapo walishinda 4-1.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pogba akicheza kusherehekea bao lake la kwanza mechi dhidi ya AFC Bournemouth ambapo walishinda 4-1.

Kiungo wa kati wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil, 30, amesema hataihama klabu yake ya Arsenal kwa mkopo mwezi huu wa Januari. Badala yake, amesema yuko tayari kusalia kupigania nafasi yake katika kikosi. (ESPN)

Juventus wamewasilisha ofa kwa kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 28, ambapo wanataka kumpa mkataba wa miaka minne ambapo atakuwa analipwa £138,000 kila wiki. (Tuttosport kupitia The Sun)

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anawakosea heshima wapinzani wake kwa jinsi anavyosherehekea kufunga mabao, hilo kwa mujibu wa kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea Claude Makelele. Pogba amekuwa akisherehekea kufunga mabao kwa kucheza ngoma, lakini Makelele anaamini amevuka mipaka. "Inaudhi sana. Namshauri Pogba. Nataka kumwambia, 'Sikiliza, nenda kama hivyo katika chumba cha kubadilishia mavazi, sio sasa [uwanjani]. Inaudhi sana. Mnashinda 4-0, kisha unacheza ngoma hapa mbele yangu," amesema Makelele (Daily Mirror)

Mesut Ozil

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Ufaransa Adrien Rabiot hana mpango wowote wa kuhamia Tottenham kwa sababu anaichukulia klabu hiyo kuwa ya chini ya kiwango chake kama mchezaji. Mchezaji huyo wa miaka 23 hata hivyo bado anataka kuihama PSG. (ESPN)

Mwenyekiti na mmiliki wa Huddersfield Dean Hoyle hana nia ya kuiacha klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England iendeleze kuteleza na kushushwa daraja na ameahidi kuwanunua wachezaji zaidi Januari. (Daily Mail)

Kipa wa Burnley na England Tom Heaton, 32, anasema ameweka pembeni mawazo yake ya kutaka kuihama klabu hiyo baada ya kuchezeshwa kikosi cha kuanza mechi mara ya kwanza katika miezi 15. (Lancashire Telegraph)

Chelsea wamekataa ofa ya zaidi ya £20m kutoka kwa Bayern Munich wanaomtaka winga wa England anayechezea timu ya taifa ya vijana wasiozidi miaka 19 Callum Hudson-Odoi, 18. (Sky Sports)

Meneja wa Cardiff City Neil Warnock anatafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Dundee anayetokea Finland Glen Kamara, 23. (Herald)

Callum Hudson-Odoi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Callum Hudson-Odoi alijiunga na Chelsea mwaka 2007

Manchester City wanakaribia kupata sajili ya kinda wa miaka 15 anayecheza kwa mguu wake wa kushoto Oscar Tarensi kutoka Uhispania. Oscar huichezea Espanyol. (Sport)

Chama cha Soka cha England kinataka kumhoji mshambuliaji wa Southampton Charlie Austin baada yake kuonekana akionesha ishara ya V kwa mashabiki baada ya klabu hiyo kushindwa na Manchester City. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane amesema huwa anacheza akiwa na kidubwana cha kielektroniki begani, na kwamba kuwadhihirishia watu kwamba walikosea kumhusu ni jambo linalompa hamasa zaidi. (Daily Telegraph)

Harry Kane celebrates scoring for Tottenham

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Harry Kane ni mchezaji wa pili kutimiza mabao 100 Ligi ya Premia haraka zaidi (mechi 141) baada ya Alan Shearer (124)

Ligi ya Premia wanataka kufanya uteuzi wa haraka baada ya Susanna Dinnage kubadili mawazo yake ya kutaka kuwa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo. Afisa wa BBC Tim Davie na mkurugenzi wa mikakati wa ITV Tom Betts ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu. (Guardian)

Bora kutoka Jumatatu

Isco

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Isco amesema haondoki Real Madrid Januari

Kiungo wa kati wa Real Madrid Isco, 26, amepuuzilia mbali uwezekano wake wa kuhamia klabu ya Chelsea ya England. Amesema hataondoka Bernabeu wakati wa kipindi cha kuhama wachezaji Januari. (Deportes Cuatro, kupitia Metro)

Manchester City wanamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto wa Real Betis Junior Firpo lakini wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Real Madrid ambao pia wanataka saini ya mchezaji huyo mwenye miaka 22. (Mirror)

Mshambuliaji wa Liverpool Dominic Solanke, 21, amefanyiwa vipimo vya matibabu katika klabu ya Crystal Palace huku akikaribia kuhamia Selhurst Park kwa mkopo. (Mail)

Kiungo wa kati wa Chelsea Tiemoue Bakayoko, 24, amesema yuko radhi kusalia AC Milan hata baada ya kipindi chake cha kuwa na klabu hiyo ya Italia kwa mkopo wa msimu mmoja kukamilima mwisho wa msimu. (MilanNews, kupitia Mail)

Tiemoue Bakayoko

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bakayoko alichezea Chelsea mechi 43 msimu uliopita

Mchezaji anayenyatiwa sana na Liverpool ambaye kwa sasa Borussia Dortmund Christian Pulisic, 20, anaonekana kukaribia kujiunga na Chelsea kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na msambuliaji wa zamani wa Marekani Eddie Johnson kwenye mitandao ya kijamii. (Calciomercato)

Klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani imejitosa kwenye mbio za kutaka kumnunua winga wa Chelsea mwenye miaka 18 Callum Hudson-Odoi. (Kicker)

Christian Pulisic

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Christian Pulisic