AFCON 2019: Uganda wafuzu kwa kuwashinda Cape Verde 1-0

Timu ya taifa ya Uganda, the Cranes sasa ndiyo ya kwanza kufuzu kutoka kundi L kwa mechi za Taifa Bingwa Barani Afrika AFCON, baada ya kuwashinda Cape Verde bao 1-0 uwanja wa taifa wa Nambole mjini Kampala.

Baada ya miaka 38 ya kushindwa kufuzu kwa mechi za AFCON, hii itakuwa mara ya pili Uganda Cranes kushiriki mechi za kuwania kombe la Taifa Bingwa Barani Afrika ambalo litaandalkiwa nchini Cameroon mwaka ujao.

Uganda sasa ina pointi 11. Tanzania itachukua nafasi ya pili ya kundi L ikiwa wataishinda Lesotho

Ikiwa watafanikiwa huko Maseru, Tanzania watasherehekea ushindi wao wa pili wa kufuzu kwa kombe la AFCOMN na wa kwanza tangu 1980.