Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 27.09.2018: Pogba, Mourinho, Ramsey, Foden, Moyes, Fabinho
Wachezaji wakuu kadhaa wa Manchester United wamekasiriwa na usimamizi wake meneja Jose Mourinho. Mreno huyo hivi majuzi alimuambia kiungo wa kati Paul Pogba kuwa hatakuwa nahodha wa klabu tena. (ESPN)
Pogba na Mourinho walijibizana wakati wa mazoezi siku ya Jumatano kwa sababu Mourinho alifikiri mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alichapisha video iliyomunyesha akicheka wakati Manchester United ilishindwa na Derby katika kombe la EFL. (Sun)
Pogba aliuambia usimamizi wa United karibu miezi miwili iliyopita kuwa anataka kundoka Old Trafford. (Telegraph)
Naibu mwenyekiti wa United Ed Woodward amemuunga mkono Mourinho na hafikiri kumfuta meneja huyo mweny miaka 55. Hata hivyo wachezaji kadhaa wanataka kuhama mwisho wa msimu ikiwa Mourinho atabaki. (Star)
Kiungo wa kati Aaron Ramsey ataondoka Arsenal msimu ujao baada ya mazungumzo ya mkataba kuvunjika. Mchezaji huyo mwenye miaka 27 raia wa Wales yuko awamu ya mwisho ya mkataba wake na amehusishwa na Chelsea na pia Juventus. (Mirror)
Manchester City wanataka kiungo wa kati Muingereza Phil Foden 18, kusaini mkataba wa muda mrefu. (Mail)
Arsenal wanamfuatilia mlinzi wa Everton Ryan Astley. Mchezaji huyo mwenye miaka 16 alianza kuichezea klabu ya wachezaji wa chini ya miaka 23 mwezi Machi. (Mirror)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema itachuakua hadi miezi sita kwa kiungo wa kati Mbrazil Fabinho kuelewa mfumo wa kucheza wa klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye miaka 24 alijiunga na Liverpool kutoka Monaco msimu huu na alicheza Jumatano katika kombe la Carabao ambapo walishindwa na Chelsea. (Independent)
Meneja wa Leicester Claude Puel anasema kiunga wa kati nyuma raia wa Uturuki Caglar Soyuncu, 22, hajaanza kucheza kwa sababu ya kutojua lugha ya kiingereza hali ambayo inafanya iwe vigumu kuwasiliana na wachezaji wenzake. (Leicester Mercury)
Everton wanammezea mate beki mwenye miaka 20 wa Porto raia wa Brazil Eder Militao, ambaye pia anaweza kucheza kama beki na kiungo cha kati. (UOL - in Portuguese)
Barcelona wako makini kumsaini kiungo wa kati wa Ajax Frenkie de Jong, 21, licha ya Tottenham na Manchester City kuonyesha dalili za kummezea mate mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi. (Talksport)
Meneja wa zamani wa Manchester United na Everton David Moyes yuko atika orodha ya kuchukua usukani wa Nantes. Hajakuwa na kazi tangu aondoke West Ham mwisho wa msimu uliopita. (Mirror)
Wing'a wa Brentford Mhispania Sergi Canos, 21, anasema alikataa ofa kutoka Liverpool kusainia mkataba wa muda mrefu mwaka 2016. (Guardian)
Mlinzi wa Bournemouth Jack Simpson, 21, anasema amefurahishwa na nia kutoka Rangers kutaka kumsaini lakini raia huyo wa Uingereza anasema sasa anataka kubaki katika klabu hiyo ya Ligi ya Premier.
England watawaunga mkono Ujerumani wakati Uefa inakutana kumchagua muandalizi wa Euro 2024. (Times - subscription required)
Stan Kroenke amekamilisha kuinunua Arsenal. Mmarekani huyo alikubali kuinnuua kwa pauni milioni 60 na Alisher Usmanov mwezi Agosti na sana ndiye mmiliki wa hisa zote. (Evening Standard)
Bora Zaidi Kutoka Jumatano
Rais wa Real Madrid Florentino Perez anaamini mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 33, siku moja atarudi katika klabu hiyo. Ronaldo alijiunga na Juventus mwezi Julai baada ya miaka tisa huko Bernabeu. (ESPN)
Ronaldo na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 31, wamejikuta kwenye mzozo baada ya kukosa kufika kwenye sherehe za tuzo za Fifa. (Marca via Express)
West Brom wanatarajiwa kumsaini wing'a wa zamani wa Crystal Palace Bakary Sako, 30, wiki hii. Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Mali amekuwa bila ajenti tangu akatae ofa ya mkataba kutoka Palace. (Sky Sports)
Arsenal wanammezea mate wing'a wa Rennes mwenye miaka 20 raia wa Senegal Ismaila Sarr ambaye amefananishwa na mchezaji wa Barcelona Ousmane Dembele. (Mirror)
Mmililki wa Chelsea Roman Abramovich anahitaji sio chini ya pauni bilioni 3 kuweza kuiuza klabu hiyo. (Bloomberg)
Msaidizi wa Chelesea Gianfranco Zola anaaminia wing'a Mbelgiji Eden Hazard, 27, hajafikia kiwango chake cha juu zaidi na anaweza kuwania tuzo za juu kwenye kandanda. (Telegraph)
Mkurugenzi wa kiufundi wa shirikisho la FA Dan Ashworth, 47, yuko kwenye mazungumzo kuhusu wajibu kama huo uko Brighton. (The Guardian)