Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mashabiki wa soka kuanza kuingia uwanjani Misri
Waziri wa michezo wa Misri Ashraf Sobhy ametangaza kuruhusu mashabiki wa kandanda kuingia uwanjani katika michezo ya ligi ya nchini Misri
Ruksa hiyo ikiwa ni mara ya kwanza toka mwaka 2012.
Mashabiki wa kandanda walifungiwa kuingia uwanjani toka mwezi Februari 2012 baada ya mashabiki 74 wa Al Aly kufariki
Wapenda soka wataanza kuingia viwanjani kuanzia tarehe 1, ya mwezi ujao na Waziri huyo wa michezo amesema watazamaji hawatakiwi kuzidi 5000 katika kila mchezo.