Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 13.08.2018: Pogba, Karius, Rabiot, Mario, Norwood, Rojo, Denayer, Bakayoko

Chanzo cha picha, Getty Images
AC Milan wanamtafuta kiungo wa kati wa Chelsea mwenye miaka 23 Tiemoue Bakayoko kwa mkopo wa msimu wote kabla ya kumpa mkataba wa kudumu. (Sun)
Barcelona itamwinda Paul Pogba baada ya msimu wa joto wa kununua wachezaji kukamilika tarehe 31 Agosti kufuatia kukubali kuwa Manchester United hawatamuuaza mchezaji huyo mwenye miaka 25 raia wa Ufarasa mwezi huu. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kipa wa Liverpool Loris Karius, 25, anawindwa na Besiktas. Klabu hiyo wa Uturuki imekuwa na mpango wa kumsaini Mjerumani huyo kwa mkopo wa msimu wote. (Sun)
Beki wa Manchester City mwenye miaka 23 Jason Denayer amekataa kuondoka kwa mkopo kwa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ubelgiji anataka kuhamia klabu ya Uturuki ya Galatasaray. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images
Cristiano Ronaldo amewashauri Juventus kumuendea kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 raia wa Serbia amehusishwa na Manchester United na Chelsea. (Star)
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrina Rabiot, 23, amekataa ofa ya kusaini upya mkataka wake na mabingwa hao wa Ligue 1. Mkataba wa kwanza wa Mfaransa huyo unakamilika mwisho wa msimu. (L'Equipe)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlinzi wa Schalke Mjerumani Thio Kehrer, 21, anatarajiwa kujiunga na Paris St-Germain baada ya mkataba wa pauni milioni 33 kuafikiwa. (Guardian)
Real Betis watatoa ofa kwa mchezaji wa Inter Milan mwenye miaka 25 Joao Mario. Kiungo huyo wa kati alicheza mara 14 akiwa kwa mkopo huko West Ham msimu uliopita na kuichezea Ureno kwenye Kombe la Dunia. (Mundo Deportivo)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Watford Mfaransa Abdoulaye Doucoure, 25, ameonyesha dalili kuwa huenda akaihama klabu hiyo siku za usoni. (Watford Observer)
Sheffield United huenda wakamsaini Oliver Norwood, 27, kutoka Brighton na Hove Albion mwezi Januari baada ya kukubaliana kwa mkopo na mchzeaji huyo wa Ireland Kaskazini. (Sheffield Star)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanaripotiwa kwenye kwenye mazungumzo na Fenerbahce kuhusu makubaliano na mlinzi mwenye miaka 28 raia wa Argentina Marcos Rojo. (Mirror)
Mshambuliaji raia wa Scotland Ross McCormack, 31, na mlinzi Muingereza Micah Richards, 30, wataachiliwa kutoka mikataba yao na Aston Villa. (Birmingham Mail)
Bora Kutoka Jumapili
Klabu ya Real Madrid inajiandaa kutoa kiasi cha paundi za uingereza milioni 200 kwaajili ya kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji Eden Hazard. (Express).

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid pia inalenga kumsajili kiungo mchezeshaji wa kimataifa wa Denmark na klabu ya Tottenham ya Uingereza, Christian Eriksen, ikiwa kiungo wake mwenye umri wa miaka 32 raia wa Croatia Luka Mondric ataamua kuondoka kujiunga na Inter Milan. (Sun)
Mlinda mlango wa klabu wa Atletico Madrid Jan Oblakm mwenye umri wa miaka 25 amekataa kujiunga na klabu ya Chelsea licha ya timu hiyo kufikia dau la kuvunja kipengele cha mkataba wake cha paundi milioni 90. (sunday Times)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Riberto Martinez na msaidizi wake Thierry Henry wamo kwenye orodha ya kuziba nafasi ya kocha wa klabu ya Leicester City Claude Puel ambaye ana mechi mbili za kunusuru kibarua chake. (Sunday Mirror).
Beki wa kushoto wa klabu ya Leicester City ben Chilwell mwenye umri wa miaka 21, amesema mchezaji mwenzake raia wa Uingereza Harry Maguire aliyekuwa akihusishwa na kuhamia kwenye klabu ya Manchester United, atasalia kwenye timu yake mpaka mwishoni mwa msimu na hata ondoka kwenye dirisha la usajili la mwezi January. (Daily Star on Sunday).












