Manchester United ndio timu yenye bahati zaidi nayo Liverpool ikiwa timu iliokosa bahati zaidi EPL

Utafiti unasema Liverpool ingekuwa mshindi kwa kuwa ilipaswa kupatiwa penati dhidi ya Manchester United

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Utafiti unasema Liverpool ingekuwa mshindi kwa kuwa ilipaswa kupatiwa penati dhidi ya Manchester United

Liverpool hawakuwa wenye bahati kwenye ligi kuu ya England msimu uliopita wakati Manchester wakiwa ndio kubahatika zaidi, utafiti unaeleza.

Ilianguka kwa alama 12 kwenye mechi wakiwa wameathiriwa na maamuzi yasiyo sahihi, penalti, kadi nyekundu na magoli yaliyokataliwa, umeeleza utafiti uliofanywa na mtandao wa habari za michezo wa ESPN, Chuo kikuu Bath na kampuni ya teknolojia ya mawasiliano, Intel.

Manchester City ilibaki kileleni kwenye matokeo mbadala baada ya utafiti.

Hata hivyo, utafiti umebaini kuwa Huddersfield ilishuka badala ya Stoke kutokana na 'makosa'kwenye maamuzi.

Imeelezwa kuwa Brighton wangemaliza wakiwa nafasi sita juu mpaka nafasi ya tisa na kujipatia kitita zaidi cha pauni milioni 11.5.

Leicester ingemaliza nafasi ya 14 badala ya tisa, ikimaliza msimu kwa kuweka kibindoni pauni milioni 9.7.

Liverpool iliyokuwa nafasi ya nne ingekuwa ya pili kubadilishana na United na vinara wa City wangekuwa na alama 97.

Jedwali mbadala liliundwaje?

Jopo lililofanya utafiti lilifanyia tathimini picha za video za kila mchezo wa ligi kuu ya mwaka 2017-2018 wakitazama mambo yafuatayo:

  • Magoli ambayo yangekataliwa
  • Kukataa magoli kimakosa
  • Penalti zilizotolewa kimakosa (zilizosababisha magoli)
  • Penalti zilizofaa kutolewa lakini hazikutolewa
  • Kadi nyekundu zilizotolewa kimakosa
  • Kadi nyekundu zilizopaswa kutolewa lakini hazikutolewa
  • Goli la kujifunga

Ikiwa matukio yatabainika, na matokeo ya mechi yalikisiwa.Pia mambo mengine yaliangaliwa kama nguvu ya timu, mfumo wa uchezaji na faida ya kucheza nyumbani.

Mfano: Mchezo wa suluhu ya bila kufungana kati ya Liverpool na Manchester United katika uwanja wa Anfield, Liverpool walipaswa kupata penati katika dakika ya 63 na kuwa washindi wa goli 1-0

Baada ya mchakato mzima, jedwali la mbadala wa matokeo lilichorwa kwa ajili ya matokeo ambayo yangepaswa kuwa

Matokeo haya yanamaanisha kuwa madhara ya kwenye mchezo yawe mazuri au mabaya hutegemea maamuzi ya mwamuzi wa mchezo.