Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mshambuliaji nyota wa Senegal Demba Ba abaguliwa China
Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle and Chelsea Demba Ba amekumbwa na kisa cha kubaguliwa wakati wa mechi za Chinese Super League, kulingana na meneja wake Wu Jingui.
Nyota huyo mwenye miaka 33 alihusika kwenye majibizano makali na mchezaji wa Changchun Yatai kwenye mechi iliyotoka sare ya 1-1 siku ya Jumamosi.
Ba, ambaye pia aliichezea West Ham alijiunga tena na Shenhua mwezi Juni.
"Kote dunian imesisitizwa kuwa kusiwe na matamshi yoyote ya kuwabagua wanamichezo weusi
"Ligi ya Chinese Super ina wachezaji wengi wa rangi tofauti. Ni lazima tuwaheshimu washindani wetu na kusiwe na ubaguzi."
Klabu ya Italia ya Besiktas iliandika katika twitter ikimuunga mkono mchezaji wake wa zamani: "Hapana kwa ubaguzi na hauko peke yako".