Mali ya familia ya mkosoaji wa Rais Kagame yauzwa Rwanda

Mamlaka nchini Rwanda zimeuza mali ya familia ya mwanasiasa aliye kizuizini ambaye pia ni mkosoaji mkuwa wa Rais Paul Kagame.

Diane Rwigara alizuiwa kuwania urais mwaka uliopita na baadaye kakamatwa kwa madai ya udanganyifu na kuchochea mapinduzi ya serikali.

Halmashauri ya kukusanya ushuru nchini Rwanda iliuza mashine kutoka kwa biashara ya familia ya tumbaku kwa takriban dola milioni 2 katika hatua ya kulipia kodi familia hiyo inaripotiwa kudaiwa ya dola milioni 7.

Familia hiyo inasema hatua hiyo ya kuuza mali na mashtaka dhidi yake dhidi yake imechochewa kisiasa.

Mauzo ya awali ya biashara za familia ya Rwigara ya tumbaku yalileta dola milioni 595.

Bi Rwigara na mtetesi maarufu wa haki za wanawake nchini Rwanda na familia yake inasema matatizo yake yalianza wakati aliamua kuwania urais.

Hakufaulu kuwania na alipigwa maruku baada ya uchunguzi kubaini kuwa Bi Rwigara alikuwa amekiuka sheria kwa kukusanya sahihi bandia kuunga mkono kugombea kwake.

Bi Rigwara alikamatwa pamoja na mama yake Adeline Rwigara Septemba 2017 nyumbani kwake kwenye mji mkuu Kigali.

Mama yake naye anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea mapinduzi ya serikali.

Rais Kagame alishinda uchaguzi wa mwaka uliopita kwa asilimia 98.63 ya kura.

Amesifiwa kwa kuleta mafanikio ya kuichumi nchini humo tangu yafanyike mauaji ya kimbari mwaka 1994.