Kombe la Dunia 2018: Nigeria wasema wako tayari kukabili Croatia

Chanzo cha picha, AFP
Bara la Afrika linatarajiwa kuona iwapo Nigeria watajizolea ushindi baada ya Misri na Morocco kushindwa mechi zao za kwanza jana.
Super Eagles watakutana na Croatia kutoka bara Ulaya saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.
Odion Ighalo huenda aanze kwenye kikosi cha Nigeria siku yake ya kuzaliwa ya 29, huku Wilfred Ndidi naye akitarajiwa kuwa sawa kucheza baada ya wasiwasi kuhusu misuli yake ya paja.
Beki wa Nigeria Leon Balogun huenda asicheze baada ya kukosa mazoezi Alhamisi.
Croatia wana wachezaji watatu wenye uzoefu mkubwa ambao wanatarajiwa kuanza mechi: Luka Modric, Ivan Rakitic, Vedran Corluka na Mario Mandzukic.
Mechi muhimu kwa timu zote mbili
Kundi D, lina Iceland na Argentina na limekuwa likielezwa na wengi kuwa Kundi la Kifo, na mechi hii ni muhimu sana kwa matumaini ya Croatia na Nigeria kusonga mbele.
Nigeria ndio walioorodheshwa wa chini zaidi katika orodha ya viwango vya soka ya Fifa lakini wamekosa michuano saba ya Kombe la Dunia iliyopita mara moja pekee.
Iceland nao ni mara yao ya kwanza kucheza Kombe la Dunia.
Super Eagles walifika hatua ya 16 bora 1994, 1998 na 2014, ingawa ushindi wao kwenye kundi dhidi ya Bosnia-Herzegovina mwaka 2014 ulikuwa ushindi wao wa kwanza kabisa katika michuano hiyo tangu michuano iliyoandaliwa Ufaransa 1998.
Croatia walimaliza wa tatu mwaka huo, waiposhiriki mara ya kwanza kama taifa huru.
Hata hivyo, hawajafika hatua ya muondoano tangu wakati huo.
Waliondolewa hatua ya makundi 2002, 2006 na 2014.

Chanzo cha picha, AFP
Kiungo wa Real Madrid Modric, kiungo wa Barcelona Rakitic na winga wa Inter Milan Ivan Perisic bado ni wachezaji muhimu sana kwa Croatia.
Nigeria wana kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea John Mikel Obi ambaye ni nahodha wao na wachezaji wa Ligi ya Premia Victor Moses na Alex Iwobi kikosini.
Mshambuliaji wa Croatia Nikola Kalinic amesema: "Kitu muhimuzaidi kwa sasa ni alama hizo tatu. Bila shaka tuna wachezaji wazuri sana washambuliaji na hatufai kuwa na wasiwasi. Ni muhimu sana kwamba tucheze vyema na tuwaundie nafasi washambuliaji wetu."
Kocha wa Nigeria Gernot Rohr amesema:"Nalipenda kundi hili kwa sababu tunajua jinsi ya kuwajibika wakati wa mechi kubwa kwa pamoja. Nigeria tutakuwa tayari dhidi Croatia."
MAMBO MUHIMU
Mataifa hayo mawili yalipokutana
- Croatia na Nigeria wanakutana kwa mara ya kwanza
- Croatia imewahi kuonana na timu moja tu kutoka Afrika kwenye Kombe la Dunia mwezi Juni 2014 ambayo ni Cameroon. Croatia ilishinda 4-0.
- Nigeria wamewahi kushinda mechi moja tu katika ya sita walizocheza dhidi ya wapinzani kutoka Ulaya walipoilaza Bosnia-Herzegovina mnamo 2014. (Imepoteza 4, ikatoka sare mechi 1).
Croatia
- Croatia imeandikisha ushindi mechi moja tu kati ya mechi zake saba za mwisho Kombe la dunia. (4-0) dhidi ya Cameroon 2014. (Sare mbili , imepoteza nne).
- Imekosa kufungwa goli mechi mbili tu kati ya mechi 11 zake za mwisho.
- Kunzia 2006, Croatia haijawahi kushinda mechi yake ya kwanza kombe la dunia.
- Mechi zilizoshirkisha Croatia katika makala manne ya kombe la dunia zimeshuhudia kadi nyekundu tano. (tatu kwa Croatia, mbili kwa wapinzani wake).
- Ivan Perisic amehusika kwenye nusu ya magoli ya Croatia katika Kombe la dunia lililotangulia (mabao mawili na mchango moja).
- Kocha Zlatko Dalic aliyeajiriwa kuiongoza Croatia Oktoba 2017, wanashiriki shindano kubwa kwa mara ya kwanza akiwa mkufunzi. Timu yake iliifunga Ukraine kwnye mechi yake ya mwisho ya kufuzu kwa kombe la dunia kabla ya Ugiriki kwenye mchujo.
Nigeria
- Tangu ilipofuzu kwa makala ya 1994, Nigeria imeshiriki kombe la dunia kila wakati isipokuwa mwaka wa 2006.
- Hakuna timu ya Afrika ambayo imefuzu kwa Kombe la Dunia kuliko Nigeria. Nigeria imeshiriki mara sita ikiwemo 2018.
- Kati ya mechi zake 12 zilizopita katika Kombe la Dunia, Nigeria imeshinda tu mara moja (imepoteza mechi nane na kutoka sare mechi mbili mbili).
- Ushindi wao pekee umekuja dhidi ya Bosnia-Herzegovina 2014 (1-0).
- Meneja wao, Gernot Rohr, aliyekabidhiwa kikosi Agosti 2016 anashiriki kombe la dunia akiwa mkufunzi kwa mara ya kwanza.
- Nigeria ni timu yake ya nne kutoka Afrika anayoinoa baada ya kuzifunza Gabon, Niger na Burkina Faso.
- Nigeria ndio timu yenye umri mdogo zaidi katika Kombe la Dunia mwaka huu. Kwa kadiri, mchezaji wa Nigeria ana umri wa miaka 25 na siku 336.


Croatia
Walinda lango: Danijel Subasic (Monaco), Lovre Kalinic (Gent), Dominik Livakovic (Dinamo Zagreb).
Mabeki: Vedran Corluka (Lokomotiv Moscow), Domagoj Vida (Besiktas), Ivan Strinic (Sampdoria), Dejan Lovren (Liverpool), Sime Vrsaljko (Atletico Madrid), Josip Pivaric (Dynamo Kiev), Tin Jedvaj (Bayer Leverkusen), Duje Caleta-Car (Red Bull Salzburg).
Viungo wa kati: Luka Modric (Real Madrid), Ivan Rakitic (Barcelona), Mateo Kovacic (Real Madrid), Milan Badelj (Fiorentina), Marcelo Brozovic (Inter Milan), Filip Bradaric (Rijeka).
Washambuliaji: Mario Mandzukic (Juventus), Ivan Perisic (Inter Milan), Nikola Kalinic (AC Milan), Andrej Kramaric (Hoffenheim), Marko Pjaca (Schalke), Ante Rebic (Fiorentina).
Nigeria
Walinda lango: Francis Uzoho (Deportivo La Coruna), Ikechukwu Ezenwa (Enyimba), Daniel Akpeyi (Chippa United).
Mabeki: William Troost-Ekong and Abdullahi Shehu (Bursaspor), Tyronne Ebuehi (Benfica), Elderson Echiejile (Cercle Brugge KSV), Bryan Idowu (Amkar Perm), Chidozie Awaziem (Porto), Leon Balogun (Brighton), Kenneth Omeruo (Chelsea).
Viungo wa kati: Mikel John Obi (Tianjin Teda), Ogenyi Onazi (Trabzonspor), Wilfred Ndidi (Leicester City), Oghenekaro Etebo (CD Feirense), John Ogu (Hapoel Be'er Sheva), Joel Obi (Torino, Italy).
Washambuliaji: Ahmed Musa, Kelechi Iheanacho (both Leicester City), Victor Moses (Chelsea), Odion Ighalo (Changchun Yatai), Alex Iwobi (Arsenal), Simeon Nwankwo (Crotone).













