Real Madrid wamemteua kocha wa Uhispania kumrithi Zidane

Real Madrid wamemteua mkufunzi wa Uhispania Julen Lopetegui kuwa kocha wake kwa mkataba wa miaka mitatu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Real Madrid wamemteua mkufunzi wa Uhispania Julen Lopetegui kuwa kocha wake kwa mkataba wa miaka mitatu

Real Madrid wamemteua mkufunzi wa Uhispania Julen Lopetegui kuwa kocha wake kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 51 atachukua wadhfa huo baada ya kombe la dunia ambalo linaanza mwezi Juni 14

Zinedine Zidane, ambaye aliiongoza kushinda mataji matatu ya klabu bingwa alijiuzulu mwezi Mei akisema kuwa klabu hiyo inahitaji sauti mpya.

Lopetegui awali aliifunza Porto kwa miaka miwili , kabla ya kuchukua uongozi wa timu ya taifa mwezi Julai 2016.

Raia huyo mwenye umri wa miaka 51 atachukua wadhfa huo baada ya kombe la dunia ambalo linaanza tarehe 14 Juni.

Akiwa kipa wa zamani Lopetegui aliichezea Real Madrid mara moja lakini aliichezea klabu ya Logrones mara 107.

Aliyekuwa kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane
Maelezo ya picha, Aliyekuwa kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane

Alianza ukufunzi 2003 kama naibu mkufunzi wa timu ya taifa ya Uhispania yenye vijana wasiozidi umri wa miaka 17.

Aliifunza timu ya Uhispania yenye wachezaji wasiozidi umri wa miaka 19, 20, 21 kabla ya kuelekea kuifunza klabu ya Porto.

Timu ya taifa ya Uhispania haijafungwi chini ya ukufunzi wa Lopetegui, baada ya kushinda mechi 14 na kupata droo sita katika mechi 20.

Wanaanza kampeni yao ya kombe la dunia dhidi ya Ureno siku ya Ijumaa.