Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Besiktas yatozwa faini baada ya Paka kuingia uwanjani
Klabu ya Besiktas imetozwa faini na Uefa baada ya Paka kujitosa uwanjani wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich mwezi Machi
Mwamuzi Michael Oliver alisimamisha mchezo katika kipindi cha pili cha mchezo uliochezwa Vodafone Park mpaka mnyama huyo alipoondoka.
Klabu hiyo ya Uturuki wameshutumiwa kwa ''uratibu hafifu'',na wamepigwa faini kutokana na vitendo vya mashabiki kurusha vitu uwanjani na kufunga njia za kwenye ngazi, na kusababisha kutozwa faini ya pauni (£29,880).
Bayern ilishinda mabao 3-1 usiku huo.
Ilimaliza kwa ushindi wa 8-1 kwa wingi wa magoli ya kufunga kisha kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali, huku mashabiki wa klabu hiyo ya Ujerumani ikipiga kura kuwa Paka ni mchezaji bora wa mchezo huo.
Kuanzia tarehe 4-7, chombo cha Uefa kinachoshughulikia masuala ya nidhamu kimetoa adhabu 13, ikiwemo adhabu dhidi ya Besiktas.
Siku ya Jumatatu, faini mbili zilitolewa kwa Liverpool,kiasi cha pauni 25,486 baada ya kuwasha baruti katika michezo dhidi ya Manchester City na Roma, pia kurusha vitu matukio yaliyosababisha usumbufu kwa watu na uharibifu.
Bayern Munich inalazimika kulipa pauni 21,970 kwa kuvamia uwanja na kuonyesha bango lenye ujumbe usiofaa wakati wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Reala Madrid, huku Atletico Madrid wakipigwa faini ya pauni 15,819 baada ya kuzibwa kwa njia wakati wa michuano ya ligi ya Europa dhidi ya Arsenal.
Chama cha soka Urusi kilitozwa faini ya pauni 22,000 na Fifa baada ya mashabiki kuimba nyimbo za kibaguzi wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Ufaransa mwezi Machi.