Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Atletico Madrid na Marseille zatinga fainali Europa
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger hatopata tena fursa kucheza fainali za ligi ya Europa baada ya kukubali kichapo cha 1-0 kutoka kwa Atletico Madrid.
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Diego Costa aliipachikia timu yake goli moja ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo likiondoa kabisa matumaini ya Arsenal kushiriki michuano ya UEFA mwakani kwa kupitia mashindano haya.
Antoine Griezmann alitoa pasi nzuri kwa Costa ambaye alifunga kwa ufundi.
Arsenal nusura wapate goli lakini juhudi za Aaron Ramsey hazikuzaa matunda.
Ilishuhudiwa pia nahodha wa Arsenal Laurent Koscielny akitolewa nje kipindi cha kwanza baada ya kuumia kifundo cha mguu na atakosa michuano ya kombe la dunia baadaye mwaka huu.
Atletico ambao ni mabingwa mara mbili wa michuano hii watakumbana na Marseille ambao nao wamefuzu baada ya kufungwa 2-1 na Red Bull Salzburg.
Fainali itapigwa mjini Lyon May 16.