Ian Wright: Naamini Wenger alifutwa kazi

Ian Wright kushoto na Arsene Wenger kulia
Maelezo ya picha, Ian Wright kushoto na Arsene Wenger kulia

Wenger anaondoka Arsenal mwaka mmoja kabla ya kandarasi yake kukamilika na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright anaamini kwamba alijiondoa kabla ya kufutwa kazi.

Arsene Wenger ni mtu mwenye 'kanuni, mwaminifu na muadilifu'-ndio maana ninaamini alifutwa kazi na hakujiuzulu, Wright aliambia gazeti la The Sun nchini Uingereza.

Kwa kejeli zote na matusi aliorushiwa , Arsene Wenger sio mtu ambaye angesalimu amri na kuondoka kwa hiari kabla ya kandarasi yake.

''Ni hali ngumu kwamba ilifikia hatua hii na sidhani kwamba tutajua aliyechukua hatua hii kwa sababu watajificha''.

''Siku moja anaitisha mkutano na wanahabari bila ishara yoyote na watu wakitafakari ameondoka haingii akilini''.

''Lakini Arsene ataondoka akiwa na ufanisi mkubwa. Ndio maana matokeo yoyote yale anafaa kuagwa vizuri kama mtu aliyewacha sifa kubwa katika klabu hiyo. Ufanisi wote huu unatokana na yeye''.