Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Antonio Conte : Nafurahia' kusalia Chelsea, hakuna mgogoro wowote
Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte amesisitiza kuwa anafurahia kusalia katika klabu hiyo licha ya uvumi kwamba uhusiano na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abrahamovic umedorora.
Conte mwenye umri wa miaka 48 aliiongoza Blues kushinda taji la Uingereza msimu uliopita na kufikia sasa wako katika nafasi ya tatu , wakiwa pointi 15 nyuma ya viongozi wa ligi Manchester City.
Abrahamovic amekasirishwa na matamshi ya kocha huyo kwamba hakuhusishwa katika kuchagua wachezaji watakaojiunga na klabu hiyo msimu huu.
''Ningependelea kuendelea kufanya kazi na wachezaji wangu'', alisema Conte.
''Nafurahi kujaribu kila simu kuweka bidii katika kazi yangu'' .
''Ningefurahi sana iwapo ningepeta wachezaji wapya.Narudia kila mara. Mimi ndiye mkufunzi''.
''Jukumu langu ni kujaribu kutoa matokeo bora ,kujaribu kuwaimarisha wachezaji wangu katika klabu hii''.
Siku ya Jumatano, kufuatia Chelsea kushindwa na Arsenal , Conte aliwaambia maripota kwamba klabu hiyo ndio inayochagua kila mchezaji katika sera yao ya uhamiaji.
Matamshi hayo yalisababisha mgogoro katika klabu hiyo na kwamba naibu wake Carlo Cudisini ndio anayewasiliana na bodi ya timu hiyo kwa niaba yake.