Ni nani mkali zaidi kati ya Lionel Messi, Radamel Falcao, na Alvaro Morata?

Chanzo cha picha, Getty Images
Huku wachezaji watatu wakiwa wamefunga mabao sita kwenye mechi 6, mbio za kushindania kiatu cha dhahabu zinaashiria kuwa zitakuwa mbio kali sana.
Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, kijana mpya wa Chelsea Alvaro Morata na Romelu Lukaku wa Manchester United wako kileleni kwa ufungaji wa mabao.
Lakini wako katika kiwango kipi na mawiji wengine wa Ulaya?
Wale wanaowania kiatu cha dhahabu barani Ulaya
Ni mwezi wa pili wa msimu na wachezaji wawili tayari wamefunga mabao kumi na zaidi.
Mshambuliaji wa Monaco Radamel Falcaoa, amefunga mabao 11 katika mechi saba za Ligue 1, huku Paulo Dybala, akiifunga Juventus mabao 10 kwenye mechi sita za Serie A.
Kwenye La Liga, Lionel Messi anaongoza kwa ufungaji kwa mabao tisa katika mechi sita.
Ince, Redmond... Ronaldo?

Chanzo cha picha, Getty Images
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Tom Ince wa Huddersfield na Nathan Redmond wa Southampton wana kipi kwa pamoja?
Wote wako kwenye kikosi cha wacahwa wanlioana matyzuaia makuwna wangai wa uigumngaji wa mabao
Redmond alipiga mikwaju 21 katika mechi sita bila kufunga bao.
Ronaldo haonekani kufurahishwa na kasi ya Messi na matatizo yake ya kufunga mabao yanaendelea.
Nohodha huyo wa kikosi cha Ureno hajafunga bao hata moja msimu huu licha kujaribu mara 18 ,12 yakiwa kwenye mechi moja.












