Tetesi za soka Ulaya Jumatano 06.09.2017

Manchester City kuna uwezekano mkubwa kwamba hawatawasilisha dau ya zaidi ya £20m kutaka kumchukua mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, mwezi Januari. (The Sun)

Mlinda lango wa Manchester United David de Gea, 26, amemsihi beki wa Real Madrid Sergio Ramos kujipangia uhamisho wake kutoka Bernabeu. (Diario Gol)

Kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 25, hakuwa anaondoka kwa vyovyote vile kutoka Liverpool majira ya joto yanayomalizika kwa sasa, meneja mkurugenzi wa zamani wa klabu hiyo Christian Purslow amesema. (Sky Sports)

Diego Costa, 28, amerejea London anapojiandaa kufikisha tamati muda wake Chelsea na kupanga kuhamia klabu yake ya zamani Atletico Madrid. (Marca)

Wenzake mshambuliaji huyo wa Uhispania wanaamini kwamba bado anafikiria uwezekano wake kurejea katika klabu hiyo na kukubali adhabu kutokana na juhudi zake za kutaka kushurutisha kuhama kwake (Daily Telegraph)

Lakini duru za Chelsea zinasisitiza kwamba mshambuliaji huyo hajafika London bado. (Mirror)

Liverpool wamekataa kukubali ombi la Emre Can kwamba kuwe na kifungu cha maelezo ya kumfungua kwenye mkataba kwenye mkataba wowote mpya atakaoutia saini. Mchezaji huyo wa miaka 23 amesalia na mwaka mmoja pekee kwenye mkataba wake wa sasa. (Daily Star)

Vincent Janssen, 23, mambo yake kwisha Tottenham baada ya mshambuliaji huyo wa thamani ya £17m kukataa kuondoka klabu hiyo siku ya mwisho ya kuhama wachezaji. (Mirror)

Mkuu wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amedai kwamba Inter Milan hawakuwasilisha dau yoyote kutaka kumchukua kiungo wa kati wa Chile wa miaka 30 Arturo Vidal majira ya sasa ya joto. (Premium Sport)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Blaise Matuidi, 30, alikataa maombi ya kumsajili kutoka kwa Manchester United, Arsenal na Manchester City na kuamua kujiunga na Juventus kutoka Paris St-Germain kipindi cha kuhama wachezaji kilichomalizika majuzi. (France Football)

Kiungo wa kati Andres Iniesta, 33, atatia saini mkataba mpya Barcelona, rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu amesema. (Mundo Deportivo)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Brazil Julio Baptista, 35, naye anatarajiwa kujiunga na klabu ya ligi ya Championship Bolton bila malipo yoyote. (The Sun)

Mshambuliaji wa Everton Henry Onyekuru, 20, ambaye alitumwa kwa mkpo Anderlecht majira ya sasa ya joto, amesema hana majuto kwamba alikataa kuhamia Celtic. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati Josh Wright, 27, ambaye hajafungwa na mkataba wowote kufikia sasa anafanya mashauriano na Southend United kuhusu uwezekano wa kuhamia klabu hiyo ya League One. (Sky Sports)

Afisa mkuu mtendaji wa Aston Villa Keith Wyness amesema klabu hiyo ilikaribia sana kufanikiwa kusajili wachezaji wawili "nyota" kutoka Ligi ya Premia siku ya mwisho ya kuhama wachezaji England. (Birmingham Mail)