UEFA: Arsenal v Bayern Munich; Man City v Monaco; Leicester v Sevilla

Bayern Munich v Arsenal

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arsenal walilaza Bayern 2-0 nyumbani msimu uliopita lakini wakachapwa 5-1 uwanjani Allianz Arena

Arsenal wamepangwa kucheza na Bayern Munich, Leicester City watakutana na Sevilla nao Manchester City wakabiliane na Monaco katika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Gunners wamecheza dhidi ya mabingwa hao wa Ujerumani mara nne katika misimu mitano iliyopita.

Walimaliza wa pili nyuma ya Bayern katika hatua ya makundi msimu uliopita.

Leicester City, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England, wana kibarua dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi ndogo ya Ulaya, Europa League Sevilla ya Uhispania.

Wapinzani wa Manchester City Monaco walilaza Tottenham mara mbili katika Kundi E.

Droo kamili:

  • Manchester City (Uingereza) v Monaco (Ufaransa)
  • Real Madrid (Uhispania) v Napoli (Italia)
  • Benfica (Ureno) v Dortmund (GER)
  • Bayern (Ujerumani) v Arsenal (Uingereza)
  • Porto (Ureno) v Juventus (ITA)
  • Leverkusen (Ujerumani) v Atlético (Uhispania)
  • Paris (Ufaransa) v Barcelona (Uhispania)
  • Sevilla (Uhispania) v Leicester (Uingereza)