Sergio Aguero: Nyota wa Manchester City kukosa mechi nne

Sergio Aguero akimkabili David Luiz

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Manchester City walilazwa 3-1 nyumbani na Chelsea Jumamosi

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amepigwa marufuku kucheza mechi nne baada yake kufukuzwa uwanjani kwa uchezaji mbaya mara ya pili msimu huu.

Aguero, 28, alifukuzwa uwanjani kwa kumchezea visivyo beki wa Chelsea David Luiz wakati wa mechi ambayo City walilazwa 3-1 nyumbani Ligi ya Premia siku ya Jumamosi.

Mshambuliaji huyo wa Argentina alikuwa ameadhibiwa tena mwezi Agosti alipopewa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo mchezaji wa West Ham Winston Reid.

Atakosa mechi za City dhidi ya Leicester, Watford, Arsenal na Hull.

Mwenzake wa City Fernandinho pia alifukuzwa uwanjani alipokabiliana na Cesc Fabregas baada ya madhambi hayo ya Aguero na amepigwa marufuku kucheza mechi tatu.

Wachezaji wengine wa City walikabiliana.

Fernandinho amsukuma Fabregas

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Fernandinho anamsukuma Fabregas ambaye anaonekana kumzaba kofi
Fernandinho amsukumaFabregas

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Fernandinho anaonekana kukasirika na kumkaba kooni Fabregas na kumsukuma nyuma
Fabregas anaanguka

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Maafisa wa Chelsea wanaingilia kati, Fernandinho mara nyingine tena anamsukuma Fabregas, ambaye anaangukia mabango ya matangazo